MGOMBEA kiti cha Rais wa Marekani kupitia chama cha Republican, tajiri Donald Trump, amekataa kukubali endapo atakubali matokeo ...
MGOMBEA
kiti cha Rais wa Marekani kupitia chama cha Republican, tajiri Donald Trump,
amekataa kukubali endapo atakubali matokeo ya urais kwenye uchaguzi mkuu wan
chi hiyo utakaofanyika Novemba 8, 2016.
Trump
aliulizwa mara tatu na mwendesha mdahalo wa tatu na wa mwisho uliowakutanisha
Trump na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama cha Democrat, Hillary Clinton
alfajiri ya leo Oktoba 20, 2016.
“Utayakubali
matokeo ya Urais endapo utashindwa kwenye uchaguzi.” Aliuliza mtangazaji wa
Shirika la Habari Fox News, Chris Wallace.
Akijibu
swali hilo Trump alisema, “Nitaangalia swala hilo wakati uklifika.” Alijibu kwa
kifupi hata alipoulizwa mara tatu na mtangazaji huyo, Trump alisisitiza jibu
lake.
Vyombo
vya habari vya nchi hiyo vimekuwa vikimnukuu Donald Trump, akiwaambia wafuasi
wake kuwa mpinzani wake Bibi. Hillary Clinton ameandaa “mazingira” ya kuiba
kura.
Trump
amekuwa akishutubu kuwa mamilioni ya watu wameandikishwa kupiga kura ilihali
hawakustahili kuandikishwa akirejea
taarifa za Pew report na sehemu nyingine.
Taarifa
za Pew zimeonyesha kuwa zaidi ya marehemu milioni 1.8 wamo kwenye orodha ya wapiga kura, hata hiovyo ripoti hiyo haikusema
kuwa marehemu hao milioni 1.8 wameorodhesha kama wapiga kura, zaidi ya hapo taarifa
ya Pew imefafanua kuwa ni ushahidi kuwa mfumo wa orodha ya wapiga kura kwenye
jimbo hilo ni muhimu ukarekebishwa ili kuondoa hitilafu hiyo.
Na
kwamba hakuna ushahidi wowote wa mtapakao wa kasoro hiyo au mpango mahsusi wa
kuhujumu zoezi la upigaji kura.
Hata
hivyo mtangazaji wa Fox News, aliendelea kumbana Trump kwa kumkumbusha kuwa “KKuna
utamaduni wa miaka mingi nchini Marekani na hakika ni moja ya tunu za nchi hii
ni kubadilishana uongozi kwa amani, haijalishi ugumu na mpambano mkali wakati
wa kampeni na matokeo ya uchaguzi ndio mwisho wa kampuni ambapo aliyeshindwa
hukubali matokeo na kumtambua mshindi.
“Kwa
hivyo unasema hauko tayari kujiandaa kwa sasa kukubali juu ya misingi hiyo.”
Wallace alimuuliza tena Trump.
Trump
alijibu: “Nilichokwambia ndio hicho, nitakwambia wakati ukiwadia, nitakuacha
ukidhania sawa.”
Ingawa
mgombea mwenza wake, Gavana wa Indiana Mike Pence na bintiye Trump, Ivanka,
muda mfupi kabla ya mdahalo huo, walisema watakubali matokeo lakini Trump
mwenyewe hakutaka kujiingiza yeye mwenyewe kukubali kama ataridhia matokeo
endapo atashindwa.
COMMENTS