Mhandisi Oscar Kanyama (kushoto) kutoka mradi wa BackBone akitoa maelezo kuhusu mradi huo wa usafirishaji umeme wa kV4...
Mhandisi
Oscar Kanyama (kushoto) kutoka mradi wa BackBone akitoa maelezo kuhusu mradi huo
wa usafirishaji umeme wa kV400 kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (katikati). Wakati wa ziara ya Waziri kukagua maendeleo ya ujenzi wa
mradi huo, Julai 26, 2016 akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Singida Kulia ni Meneja
Mradi wa BackBone, Mhandisi Khalid James.
WAZIRI
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema, mradi wa ujenzi wa
njia ya kusafirisha umeme wa Kilovolti 400 kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga
utakamilika Oktoba mwaka huu 2016
Profesa
Muhongo ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleao ya
ujenzio wa mradi huo (BackBone Transmission line) wenye urefu wa Kilomita 670,
kutoka mkoani Iringa hadi mkoa wa Shinyanga.
Profesa
Muhongo ambaye kwa sasa yuko mkoani Singida, tayario amekwishakagua maendeleo
ya ujenzi mkoani Dodoma.
“
Mradi utakapo kamilika utaboresha upatikanaji wa umeme kwenye mikoa ya kanda ya
Ziwa na Kastazini mwa Tanzania,” alisema Profesa Muhongo.
Profesa
Muhongo pia alsiema, mradi huo ambao gharama zake ni Dola za Kimarekani Milioni
450, utapita hadi kwenye mipaka ya nchi jirani za Kenya na Zambia ambako
Tanzania inaweza kuuza umeme kwenye nchi hizo wakati ambapo Tanzania itakuwa na
umeme wa kutosheleza mahitaji.
Akitoa
taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini, Meneja Mradi, Mhandisi Khalid James, alisema, mradi huo umegawanyika
katika awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza Iringa-Dodoma, Dodoma-Singida, na
Singida-Shinyanga.
Mhandisi
James, amemwambia Waziri Profesa Muhongo kuwa, awamu ya kwanza ambayo ni ujenzi
wa njia ya umeme kutoka Iringa-Dodoma, ambao mfadhili mkuu ni benki ya Dunia kwa
thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 150, yenye urefu wa Kilomita 225 mradi huo
umekamilika kwa asilimia 100 na utazinduliwa Septemba mwaka huu 2016.
Aidha
Mhandisi huyo alisema, kipande cha Dodoma-Singida, tayari asilimia 80 ya ujenzi
wa mradi umekamilika. “Wafadhili wa mradi huu ni pamoja na Benki ya Maendeleo
ya Afrika, AfDB, na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), ambao wafadhili hao
wametoa jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 169. alisema Meneja mradi na
kuongeza kuwa uzinduzi wa mradi huo utafanyika Oktoba 2016.
Mhandisi
James alisema, awamu ya tatu ya mradi huo ambayo ni Singida-Shinyanga yenye
urefu wa Kilomita 228 na ambao umefadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya EU kwa gharama
ya Dola za Kimarekani Milioni 134, umekamilika kwa asilimia 99 na utazinduliwa
Oktoba mwaka huu 2016.
“Mradi
huu wa BackBone pia utahusika nauboreshaji wa vituo vya kupooza na kusambaza umeme
katika Mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga ambapo upanuzi huo unafadhiliwa
na Benki ya Maendeleo ya Korea kwa kiasi cha Dola za Marekani Milioni 36”.
Mafundi
wa Kampuni ya Joyti Structures Ltd wakiunganisha moja ya nguzo
za kusafirisha umeme zenye uwezo wa kV 400 kutoka Dodoma hadi Singida.
Baadhi
ya nguzo zilizokwishakamilika ambazo zitasafarisha umemewa kV 400 kutoka Iringa
hadi Shinyanga.
Mhandisi Joseph Mongi kutoka Kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Zuzu Mkoani Dodoma akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. SospeterMuhongo
COMMENTS