Mgeni Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji, Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Moshi, Wence...
Mgeni
Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji, Mkuu wa idara ya Utumishi
na Utawala Manispaa ya Moshi, Wenceslaus Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi
wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia Wakulima wa
AgriProFocus yanayofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika
mjini Moshi.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji waliohudhuria ufunguzi wa maonesho hayo ya siku Mbili.
Afisa
Msaidizi wa Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye
ndoto wa AgriProFocus, Hildagard Okoth akitoa maelezo kwa mgeni rasmi
Wenceslaus Lindi wakati akitembelea mabanda katika maonesho ya Wakulima
na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika
Moshi.
Afisa
Ugavi wa SEVIA,Lewis Mlekwa akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi
alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya Wakulima na
Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na
Biashara mjini Moshi.
Bwana
Shamba wa kampuni ya Agrichem Africatz Ltd ,Mrisho Yusuph akimuonesha
mgeni rasmi baadhi ya mbegu zinazotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya
wakulima.
Mgeni rasmi akiwa katika banda la East West Seed akipewa maelezo juu ya aina mbalimbali ya mbegu zinazotolewa na kikundi hicho.
Meneja
Mradi mkazi wa Farm Radio International, Joseph Sarakikya akiomuonesha
mgeni rasmi namna radio zinavyoweza kutumika katika kusaidia wakulima .
Afisa
mahusiano wa taasisi ya fedha ya Vision Fund, Elias Mlaki akitoa
maelezo kwa mgeni rasmi mara baada ya kutembelea banda la taasisi hiyo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wametembelea mabanda mbalimbali kujionea maoensho hayo ya wakulima na wafugaji.
Mmoja wa wafanyakazi katika banda la East West seed akimvisha kofia mmoja wakulima waliofika kutembelea banda hilo.
Baadhi
ya vijana walionesha kuvutiwa na kuingia katika shughuli za kilimo
wakijaribu kuangalia aina ya mbegu zinazotolewa na East West Seed
walipotembelea banda hilo.
Baadhi ya vijana walivutika zaidi katika ufugaji wa kuku wa kisasa mara baada ya kutembelea banda la Brac.
Afisa
Msaidizi wa Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye
ndoto wa AgriProFocus akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi
wa maonesho hayo.
(Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini).
COMMENTS