HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE

Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na w...




Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti mabalimbalai wamejitokeza  na vielelezo  vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo ulivyoharibika
Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii ni fomu kutoka Kituo cha Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo halali kutokana na kukosa muhuri wa tume ya uchaguzi Zanzibar.  Msimamizi wa kituo ni Khamis Mkungwa Zaidi.
Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940
A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni  namba 1926, fomu hii imepoteza uhalali kwa sababu imefutwafutwa na haina muhuri wala jina la msimamizi wa kituo.
B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii ni fomu kutoka katika kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618, Katika  jimbo la Chumbuni namba 1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu imefutwa majina ya mawakala na kupandikizwa majina mengine juu ya maandishi ya kivuli.
C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi  mbili,  fomu kutoka kiwanja cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka jimbo la Chumbuni namba 1937, fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina muhuri, maandishi yameandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi uya mara moja.  Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ni muhuri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
D. Mihuri ya kughushi
Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu ina muhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.
Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.

E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC alisema utata wa matokeo ulianza pale wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi na kuiarifu Tume dhidi ya matendo yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na mabishano yakiendelea mmoja wa wagombea akaitisha wanahabari na kujitangaza ameshinda kwa matokeo ambayo kila mmoja wetu alishangaa sana.

Ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara yake, sijui alitoa wapi Takwimu ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea wawili tu, tena ukijumlisha asilimia ni 100 inasikitisha sana. Shinikizo la kunitaka nimtangaze mshindi kinyume na taratibu lilinifanya niubebe msalaba kusimamisha na kufuta matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache za uthibitisho mwandishi haya ndio tuliyakuta. Ni nusu ya uchaguzi wote kila jimbo ulichezewa

Tumejiridhisha watu wetu watendaji wa ZEC walio apa walifanya haya, kutumia mihuri ya bandia kujaza hizi fomu kinyume na taratibu kama mnavyoona alisisitiza, Jecha kwa masikitiko akiwaonyesha waanndishi waliofika kuhoji nini kilitokea hasa.

COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE
HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE
http://www.focusmedia.co.tz/sites/default/files/u38/23801%20-%20CHONGA%20HAINA%20MHURI.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/haya-ndiyo-yaliyosababisha-uchaguzi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/haya-ndiyo-yaliyosababisha-uchaguzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy