WIZARA YA AFYA YATOA TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandi...








DSC_0063
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dkt. Rufaro Chatora
Taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini ni kama ifuatavyo; Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huu.
Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 04 hadi 10 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 615 walioripotiwa nchini kote na vifo vitatu (3).  Mikoa ambayo bado imeripoti kuwa  na ugonjwa huu ndani ya wiki moja iliyopita ni 11 kati ya 21 iliyokuwa imeripoti ugonjwa hapa nchini. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mikoa inayoongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wapya ndani ya wiki moja iliyopita ni pamoja na  Morogoro (Manispaa ya Morogoro  87, Halmashauri ya Morogoro  66), ukifuatiwa na Arusha (Arusha Manispaa 50), Singida (Iramba 40) na   Manispaa ya Dodoma ( 33).
Aidha, mikoa  iliyokuwa na maambukizi lakini  kwa muda wa wiki moja iliyopita hakukuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu ni pamoja na  Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Lindi. Vile vile mkoa wa Dar es Salaam ambako ndiko ugonjwa ulianzia na kudumu kwa muda wa miezi minne (4) haujaripoti mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015.
Mikoa ambayo ilikwisha kuwa na ugonjwa huo lakini hapajakuwepo na wagonjwa wowote kwa muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa. Pia mikoa ambayo haijawahi kutoa taarifa ya ugonjwa wa kindupindu tangu mlipuko huu uanze hapa nchini ni  Njombe, Ruvuma na  Mtwara.
Bado Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea kusisitiza kuwa, ili kudhibiti ugonjwa huo na kuokoa vifo vinavyotokana na ugonjwa huu, wananchi wanasisitizwa kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka:-
-kabla na baada ya kula
- baada ya kutoka chooni
-baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia
-baada ya kumhudumia mgonjwa
Aidha, jamii inaaswa kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, maziwa na mabwawa.
Hivyo, Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja na watendaji wake kote  nchini zinaagizwa kuendeleza juhudi za kuzuia kusambaa kwa mlipuko pamoja na kuchukua hatua stahiki za tahadhari kwa kusimamia utekelezaji wa yafuatayo:
*Ushirikishwaji wa viongozi ngazi mbali mbali, hasa ngazi za Halmashauri kwa kushirikisha madiwani na viongozi wa kata, vijiji, na mitaa.
*Mamlaka husika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni pamoja na uwekaji wa dawa ya klorini kwenye maji na kupima usalama wa maji mara kwa mara.
*Upatikanaji wa dawa za kutibu maji (Water Guard, Aqua Tabs) katika maeneo ya mlipuko.
*Juhudi kubwa ziongezwe kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya vyoo bora kwa kila kaya.
*Uelimishwaji wa Baba na Mama Lishe, na wauzaji wengine wa vyakula kuhusu kanuni za afya.
*Kusimamia utekelezwaji wa Sheria ya Afya ya Mazingira na Sheria ndogo ndogo (By-Laws).
*Uhamasishaji wa Wananchi wanaopata ugonjwa kuwahi kutumia maji ya chumvi  chumvi (ORS) na kuripoti mapema katika vituo vya huduma.
*Uboreshwaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Hitimisho
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inawashukuru wadau wote wanaoshirikiana na Serikali katika harakati za kupambana na ugonjwa huu. Aidha, Wizara inaipongeza mikoa ambayo ilikuwa na ugonjwa na sasa umetoweka au kupungua kwa kiasi kikubwa na pia kuikumbusha mikoa ambayo bado haijaathirika kuchukua hatua za tahadhari za kuzuia ili isipate mgonjwa yeyote wa Kipindupindu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WIZARA YA AFYA YATOA TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI
WIZARA YA AFYA YATOA TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEgV7lbzy51Nzg_VJ7owdAR4Mc-xhHXwt7js5pJ8PysdG17kf_GeiVC0VZv_-RRa7eCOPfJLVtXvfUaRb9WwTC3iySDZxGNoU2_428LcMJG5s28_UClbUSKfnFDS-7mqkED37inzlrq56xn0C1BT0xpupe_7F0xxTwdOQXEb=s0-d-e1-ft
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEgV7lbzy51Nzg_VJ7owdAR4Mc-xhHXwt7js5pJ8PysdG17kf_GeiVC0VZv_-RRa7eCOPfJLVtXvfUaRb9WwTC3iySDZxGNoU2_428LcMJG5s28_UClbUSKfnFDS-7mqkED37inzlrq56xn0C1BT0xpupe_7F0xxTwdOQXEb=s72-c-d-e1-ft
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/01/wizara-ya-afya-yatoa-taarifa-kuhusu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/01/wizara-ya-afya-yatoa-taarifa-kuhusu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy