DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR ES SALAAM

DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es S alaam (DAWASCO) limewakamata watu 8 wenye masham...







DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI
DAR

Shirika la Majisafi na Majitaka
Dar es Salaam (DAWASCO) limewakamata watu 8 wenye mashamba eneo la Sakoveda
Mbezi Juu wilayani Kinondoni baada ya kugundulika wakiliibia Maji shirika hilo.

Akizungumza wakati wa operesheni
ya mtaa kwa mtaa kuhakiki matumizi sahihi ya Maji kwa watumiaji wakubwa wa Maji
eneo hilo, Meneja wa Kawe, Bwana Crossman Makere alisema operesheni hiyo ni
mwanzo tu wa kutumbua uovu unaofanywa na watumiaji Maji kwa mgongo wa Ulimaji Mashamba
na uuzaji maua ulioshika kasi jijini Dar.

“Dawasco tunajiendesha kwa
kuzalisha Maji na kuhudumia wananchi na gharama zote hizo ni kutokana na mapato
yanayopatikana ndani ya shirika kutokana na Ankara ya Maji inayolipwa na mteja.

“kwahiyo inapotokea watu wanafanya
hujuma za aina yoyote ieleweke kwamba shirika linaingia hasara kubwa ambayo
haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote.
“hivyo basi tumeamua kufanya
ukaguzi wa mashamba na bustani zote za mboga ili kubaini ni kina nani
wanaohujumu shirika kwa kujiunganishia Maji kupitia njia za panya” Alisema Bwn
Makere.

Aliongeza kuwa watu hao 8
wamekamatwa baada ya kupata taarifa toka kwa wasamalia wema juu ya kuwepo kwa
maunganishio yaliyofanywa usiku wa manane ambayo yanapeleka Maji kinyemela
katika mashamba hayo yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 3.

“tumegundua maungio ya Inchi Moja
zaidi ya 2 yanayopeleka Maji kwenye mashamba hayo ambayo wanalima zaidi mboga
za majani kama mchicha na spinachi kwenye shamba hilo ambapo licha ya kuwataka
wahusika wajieleze kuhusu Maji wananyotumia kustawisha mboga hizo hawakuwa na
majibu sahihi” alisema Bwana Makere.

Kwa upande wake, Mmoja wa
wamiliki wa shamba hilo Bi Rahabu Vicent alisema tangu aanze kilimo hapo
alikuta Maji yameunganishwa na hawakujua aliyeunganisha na yeye anategemea
zaidi Maji ya Mto unaopita pembeni ya Mashamba yetu hivyo Maji ya DAWASCO anayatumia
ila kwa kiasi kidogo.

Watuhumiwa hao walipoulizwa kama
wanautaratibu wa kulipa Ankara zao kila mwezi kwa Maji ya Dawasco wanayotumia,
Bi Rahabu alisema tangu waanze kutumia Maji hayo hawajawahi kupata bili yoyote
toka DAWASCO na hawakufatilia kupata utaratibu wa kulipia kwani hata Mita ya
Maji hawana.

Kwa upande wa mjumbe wa serikali
ya Mtaa wa Sakuleda Bwn Cwell Mbeye alikiri kufahamu biashara hiyo kufanyika
katika eneo hilo na kusema wananchi walishalipigia kelele suala hilo kwani
wafanyabiashara hao walisababisha huduma ya Maji katika eneo hilo kukosekana
kutokana na wao kuhujumu miundombinu ya Maji katika eneo lao.

‘Tunaishukuru DAWASCO kuja
kufanya operesheni hii kwani tunaamini sasa kilio cha wananchi wa eneo hili
kukosa Maji kitapungua na sasa huduma hiyo itarudi baada ya wabadhilifu hao
kujulikana na miundombinu yao kukamatwa” alisema Bwn Mbeye


Kesi hiyo imefunguliwa katika
kituo cha polisi Kawe  na shauri
litapelekwa Mahakama ya Jiji kwa ajili ya hukumu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR ES SALAAM
DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3RW32VePHRYh4uz86vCahHuP_oR1JU5zYPPFlFk5KOkJgKfjugwM-_fHbwIeCVeQh33cQvuwBg7v5pWU7KnoUHFQW5lWnyjSVGp4-mvsMFnuwKc8X0IbXaGsI1BzsLNm1tSFf7JnwUdHj/s1600/index.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3RW32VePHRYh4uz86vCahHuP_oR1JU5zYPPFlFk5KOkJgKfjugwM-_fHbwIeCVeQh33cQvuwBg7v5pWU7KnoUHFQW5lWnyjSVGp4-mvsMFnuwKc8X0IbXaGsI1BzsLNm1tSFf7JnwUdHj/s72-c/index.png
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/01/dawasco-yakamata-8-wizi-wa-maji-dar-es.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/01/dawasco-yakamata-8-wizi-wa-maji-dar-es.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy