HABARI za uhakika zilizotufikia leo asubuhi zimeeleza kuwa kituo cha polisi Sitaki S hari Ukonga , jijini Dar es Salaam, kimevamiwa us...
HABARI za uhakika zilizotufikia leo asubuhi zimeeleza kuwa kituo cha polisi Sitaki Shari Ukonga, jijini Dar es Salaam, kimevamiwa usiku wa saa 5 Julai 12, 2015 na watu wasiojulikana ambapo, askari polisi wanne na raia watatu wameuawa.
Pia silaha idadi isiyofahamika bado zimeporwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo kati ya hizo zimo SMG 15, SR 6 na risasi kadhaa.
Taarifa za majirani zinaeleza kuwa watu hao waliokuwa na silaha, walianza kupiga risasi ovyo kituoni hapo ambapo, askari wanne waliokuwa zamu, waliuawa. Taarifa za ndani kutoka Jeshi la polisi zinasema, raia watatu pia waliuawa kwenye shambulio hilo akiwemo mwendesha bodaboda mmoja aliyewaleta anayesadikiwa kushirikiana na wavamizi hao.
Raia wawili waliouwa walikuwa kituoni hapo kuwawekea dhamana ndugu zao waliokuwa mahabusu.
Taarifa zaidi zinasema, wavamizi hao hawakushughulika na mahabusu na baada ya kutekeleza unyama huo waliondoka na gari, walilokuja nalo hata, wavamizi hao walimuua kwa kumpiga risasi mwendesha bodaboda waliyekuwa wakishirikiana naye wakati wa kuondoka kituoni hapo baada ya pikipiki yake kugoma kuwaka.
Majirani wanasema, milio ya risasi ilirindima kwenye eneo hilo na hali ilitulia majira ya saa 7 usiku.
Mojawapo ya pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na mtuhumiwa aliyekuwa akishirikiana na wahalifu. |
Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu ukiongozwa na gari la Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ukiwasili eneo la tukio. |
Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu akikagua kituo hicho baada ya kuwasili kituoni hapo mchana huu. |
Moja ya gari la Raia mwema aliyeuwawa wakati alipokwenda kituoni hapo kumepeleka mhalifu. |
Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu uakiongea na waandishi wa habari kituoni hapo. |
Mkazi wa jijini akipita jirani na moja ya nyumba ambapo ukuta wake ulipigwa risasi wakati majambazi hao wakisafisha njia baada ya kupora silaha nyingi kituoni hapo. |
COMMENTS