Mratibu wa maonesho ya Beauty Salons and Beast, Jan van Esch akiongea na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo yanayoanza Msasani en...
BEAUTY
SALONS AND THE BEAST
(SALUNI ZA UREMBO NA URIMBO)
(SALUNI ZA UREMBO NA URIMBO)
‘Mwisho
wa siku…sanaa ya umma…inahusu sanaa na umma. Na hilo litaendelea kuwa hivyo
pale ambapo huo umma siyo tu kikundi kidogo cha watu wanaojua na kufuatilia
sanaa, bali ni mchanganyiko wa taifa lenye matabaka, fursa tofauti, viwango
mbalimbali vya kuwa na muda wa kutosha; hivyo basi, sanaa ya umma hakika
itakuwa ni ya umma pale tu inapohusu vilivyo vya umma.’
Mwaka 2008 nilishuhudia uzinduzi wa
kile ambacho sasa kimekuwa tamasha maarufu sana la sanaa duniani lijulikanalo kama
Infecting The City, yaani ‘Kuliambukiza
Jiji’. Hili ni tamasha linaloshirikisha aina nyingi za sanaa na maonyesho
katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini na hivyo kutoa nafasi na fursa
kwa mtu yeyote kuzifikia na kuona kazi mbalimbali za sanaa. Kipindi hicho
nilikuwa ndiyo kwanza naanza mwaka wangu wa tatu wa masomo ya Shahada ya kwanza
ya Sanaa, hivyo, hata sikujua mwelekeo wangu kitaaluma na kisanii utakuwaje.
Lakini nakumbuka jinsi gani wazo la walioanzisha tamasha hilo lilivyonigusa na
kunifanya nitamani siku moja na sisi tuazime hata sehemu ndogo tu ya wazo hilo
ili kuwe na tamasha kama hilo katika jiji letu la Dar es Salaam, Tanzania. Pia
nilitamani niwe mmoja wa waandaaji wa tamasha la aina hiyo jijini Dar es Salaam
kwa kadri vionjo, uwezo na muktadha wetu utakavyoruhusu. Hatimaye mwaka huu,
ikiwa ni mwaka wa nane toka niupate ule uzoefu ulionigusa kwa mara ya kwanza,
nimefanikiwa kuifikia azma hiyo kupitia maonyesho ya Apexart Franchise
tuyaitayo “Beauty Salons and the Beast”, yaani, 'Saluni za Urembo na Urimbo.’
Tamasha
la Saluni za Urembo na Urimbo ni zao
la wasanii wawili – mimi mwenyewe, Rehema Chachage, na Jan van Esch – ambao pia
tupo kwenye menejimenti ya taasisi ijulikanayo kama Nafasi Art Space, kituo pekee
cha sanaa ya kisasa jijini Dar es Salaam. Wazo la kuwa na tamasha hili
liliibuka kufuatia hali tuionayo Tanzania, yaani: kuhudhuria maonyesho ya sanaa
kiukweli siyo utamaduni wa Watanzania walio wengi. Hivyo, ukilinganisha na raia
wa kigeni, hakuna Watanzania wa kutosha wanaohudhuria maonyesho ya utamaduni
pamoja na matukio mengine ya kiutamaduni katika vilinge vya tamaduni jijini.
Sisi kama waandaaji wa takribani asilimia 50 ya maonyesho hayo, mara kwa mara
tunajikuta tukijiuliza umma wa Watanzania uko wapi na ni kwa namna gani
tunaweza kufanya iwezekane kwa umma huo kupata fursa ya kuona sanaa na
kuwafikia wasanii.
Baada ya kubunga bongo na kutafakari
sana, tukahitimisha kuwa labda njia pekee ya kuweza kuwafikia watu wengi zaidi
ni kwa kuazima mbinu ya ‘Kuambukiza Jiji’
na kujaribu kufanya maonyesho yanayoibuka ‘papo kwa hapo’ katika maeneo ya umma
ili kuvutia mkusanyiko mkubwa wa Watanzania. Tunasema, ‘Kama hawataifuata sanaa, basi tuiachie sanaa iwafuate wao;’ na
tupo kwenye mkakati wa kuwafuata (umma wa) watazamaji wa sanaa popote pale
walipo. Katika jaribio hili la kwanza la maonyesho ya ‘papo kwa hapo’, tumeamua
kutumia saluni kama maeneo ya maonyesho baada ya kuona makala ya Beauty Salons and the Beast (yaani Saluni za urembo na Urimbo) iliyoandikwa
na Erick Mchome. Makala hiyo inaonyesha ni kwa kiwango gani saluni zimekuwa ni
biashara zinazokuja juu kwa kasi jijini Dar es Salaam ambapo tunaona kundi
kubwa la watu wa matabaka ya juu, kati na chini ya kiuchumi/kimaisha nchini
Tanzania yakitumia muda wao wa ziada humo, hasa mwisho wa wiki, yaani, wikiendi.
Hawa ndiyo aina ya watazamaji ambao maonyesho yetu yanalenga kuwafikia.
Katika jaribio hili la kwanza la
maonyesho ya ‘papo kwa hapo’, tumeona ni vyema tujaribu kwanza kutumia saluni zilizoko
katika maeneo ya karibu na tulipo, hivyo tumechagua eneo la Msasani ambalo
kiutawala ni kata katika Wilaya ya Kinondoni. Msasani pia ipo kati ya Peninsula (yaani maeneo ya Masaki/Oysterbay),
ampapo wanaishi wageni wengi pamoja na Watanzania wengi wa daraja/tabaka la
kati na la juu kiuchumi/kimaisha, na Kijiji cha Msasani ambacho zamani kilikuwa
ni kijiji cha wavuvi na mpaka sasa kina mkusanyiko mkubwa wa watanzania wa
tabaka la chini kiuchumi. Hali kadhalika ni rahisi kwa watu wengine kutoka
maeneo mengine ya Wilaya ya Kinondoni (wengi wao wakiwa ni mchanganyiko wa
tabaka la chini na la kati kimaisha/kiuchumi) kupafikia Msasani maana biashara
nyingi zinazowahudumia ziko hapo. Hivyo mazingira hayo yanatupa fursa ya
kuwafikia Watanzania wengi na wa aina nyingi ambao kwa kawaida hatuwaoni kwenye
maonyesho ya wazi ya usiku tuyafanyao katika kituo chetu cha Nafasi Art Space.
Kama walivyo wasanii wengi wanaongezeka
leo, wasanii waliochaguliwa kwa ajili ya maonyesho ya Saluni za Urembo na Urimbo wanapendelea sanaa ya umma na kuhoji
nafasi zao katika jamii kwa kutumia sanaa kuwasiliana na jamii husika kuhusu
masuala muhimu ya kijamii. Wanatumia maonyesho haya kama mbinu ya kuitoa sanaa
kwenye kuta nne za kituo cha sanaa walichokizoea na kuzipeleka nje kwa watu
ambao siyo kawaida yao kuja kwenye vituo vya sanaa. Kwa kuwafikia watu hao,
wasanii hawa pia wanapata fursa ya kusikiliza maoni mbadala kuhusu ujumbe wao
wa kisanii na hivyo kuwawezesha kukuza maono na usikivu wa vionjo na tafsiri za
Kitanzania kuhusu sanaa ya kisasa. Kupitia kitendo hiki, wasanii wanataka
kuwapa changamoto watazamaji na wao wazingatie na watazame kwa undani zaidi
mazingira waliyopo – yaani, muktadha ambao sanaa yao inapokelewa nao na
mitazamo inayoibuka humo ni masuala muhimu katika maonyesho haya. Kwa namna
fulani, wasanii hawa wanachukua nafasi ya watetezi (kupitia sanaa) wa mitazamo
mbadala inayohoji tafsiri, imani na misimamo ya jamii.
Kuna njia nyingi za kutafsiri mitazamo
na maana ya mchango wa kila msanii. Sisi kama wasimamizi wa maonyesho haya ya Saluni za Urembo na Urimbo, tumetoa
fursa kwa mtazamo na tafsiri yoyote ile ambayo wasanii wataiongezea kwenye wazo
letu la kuwa na maonyesho haya. Japokuwa kila mada ya msanii katika nafasi yake
imejikita kwenye taaluma au mfumo fulani wa sanaa, mnyanganyiko wa uzoefu wa ndani na wa nje wa wasanii wote, kwa pamoja, ni
mpana na unaakisi uzoefu wa nchi yetu na siasa zake katika mapana yake.
Maonyesho yaliyojumuishwa katika Saluni za Urembo na Urimbo ni yale
ambayo yanagusa fikra zetu na kugusia kipindi hiki na mazingira yetu ya sasa
nchini. Mengi yanagusia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 na kurejea miaka 5+ ya
Uhuru na miaka 20+ ya mfumo wa demokrasia ya kiliberali pamoja na mikanganyiko
yake, mmojawapo ukiwa ni namna ya kuzuia rushwa/ufisadi na matumizi mabaya ya
madaraka. Kwa kuzingatia upigaji kura, wasanii kwa pamoja walikubaliana tuanze
na mfumo wa maswali ya kuchagua kama mbinu ya kwanza na mada mtambuka – kama
namna ya kutathmini ambapo watu wanaulizwa wachagua jibu au majibu kutoka
kwenye orodha ya majibu, mtu hugudua kuwa mara nyingi jibu linakuwa ni majibu
yote, yaani kuna mengi ya kuchagua.
Jan
van Esch na Aika Kirei, kwa mfano, wanatumia ‘mbinu ya kutathmini kwa kutumia
maswali ya kuchagua’ kuuliza maswali kuhusu namna ambavyo wajasiriamali wadogo
wadogo na wa kati wanavyopata au kukosa fursa. Na, kama ilivyokuwa kwa baba
yake aliyekuwa Profesa wa Sosholojia na Mchambuzi wa masuala ya Kijamii na ambaye anasemekana kuwa mtu wa kwanza
kuyachezesha kikejeli maneno ya kaulimbiu ya chama tawala ya uchaguzi wa mwaka
2005, Rehema Chachage naye
anayachezea kisanii maneno hayo ya ARI, NGUVU, KASI ambayo kiuhalisia yamekuwa
kinyume chake na kuwa A, -NGU, -KA (ANGUKA) kutokana na chama hicho kushindwa
kutekeleza mambo mengi waliyoahidi. Vivyo hivyo, japo kwa mbinu tofauti, Gadi Ramadhani anatumia mwendelezo wa
maonyesho yake ya Blindfolded
(Kufungwa Macho) kuonyesha, kwa mtazamo wa kisanii, ni jinsi gani leo sisi kama
jamii tumefungwa kitambaa machoni hivyo ni kama vile tunatembea bila
kujua/kuona jinsi ambavyo mfumo tawala (wanasiasa, vyombo vya habari n.k.)
unatuhadaa.
Kwenye suala la maamuzi na kuchagua, Delphine Buysse anatumia madoli 50 yanayoning’inia kichwa
chini miguu juu na ambayo yamepakwa rangi ya kijivu kwa asilimia 50, kuonyesha
na kuchambua mtanziko wa maisha na ugumu utokanao na kuamua/kuchagua. Eneida Sanches naye analitazama suala
hilo hilo ila kwa namna tofauti. Kwa kutumia michoro ya wanaume ambao hawapo
(tena) katika maisha yake, sanaa yake inaonyesha mikanganyiko na tafakuri
kuhusu wanaume hao na uchaguzi/uamuzi wao wa kumwacha… swali lake kuu likiwa
ni; wako wapi na nini kiliwafanya waondoke/wamwache?
Cloud
Chatanda anakuja na mtazamo chanya zaidi kwenye
mada hii kwa kutumia mchanganyiko tete wa uchoraji na uchongaji kuonyesha jinsi
viumbe vya zamani visivyojulikana ambavyo kwa muda mrefu vimegana kwenye Mlima
Kilimanjaro vinaamka na kukuta Tanzania iliyo katika hali tata na kuamua
kupambana na matatizo ili kulirudisha Taifa kwenye hali yake ya asili. Hali
kadhalika Amani Abeid naye anakuja
na mtazamo chanya kwa kuonyesha shujaa anaejitokeza (kutoka Tanzania) kuikoa
dunia kutoka kwenye majanga baada ya mashujaa maarufu na wapendwao wa nchi za
magharibu kushindwa kufanya hivyo.
Onyesho la Vita Maluli, ambalo limejikita zaidi kwenye kejeli, linatumia
‘kango moko’, yaani kipande kimoja cha kanga chenye vijimaneno au vijembe,
ambapo tunaona kanga ikiwa imepata uhuru zaidi hivi karibuni baada ya kuacha
utamaduni wa kuwa tu vazi la kuvaliwa nyumbani kwa matumizi ya ndani na kuwa
pia vazi linaloonekana mitaani, likiwa limevaliwa na wanawake mchana kweupe.
Kila msanii
anajaribu, kwa namna yake ya pekee, kupaza sauti yake kuelezea yale
yanayomgusa. Kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Afrika, Tanner Methvin
anavyosema, “propaganda ni kusema hatuna mamlaka ya kujieleza kwa Uhuru. Eti
sauti zetu zinahitaji ruhusa kutoka kwa mtu au kitu fulani chenye mamlaka hayo.
Kuwa walimu wetu, wakuu wa taasis za elimu, mabosi wetu, na maofisa wa Serikali
ndiyo wanaturuhusu kucheza muziki, kuimba, kuchora, kupiga picha, kuandika, au
hata kuongea tu. Wanatuambia lini tumechaguliwa au tumeteuliwa na hapo ndipo tu
tunaposimama…Hili kwa hakika ni hekaya lakini ambayo tunashiriki kuitunga na
kuikuza kila mara tunapojibana wenyewe na kuzikimbia fursa za kuelezea visa
vyetu wenyewe.”
Rehema
Chachage (Msimamizi wa maonyesho, Beauty Salons and The Beast—Saluni za Urembo na Urimbo)
PRESS
RELEASE: LAUNCH OF BEAUTY SALONS AND THE BEAST EXHIBITION AND INTERVENTIONS
FOR
IMMEDIATE RELEASE.
The launch of ‘Beauty Salons
and the Beast’; an art exhibition featuring interventions in beauty salons and
barbershops of Msasani area, Dar es Salaam. The exhibition will feature artworks
and interventions from the following artists;
Amani Abeid (Tanzania)
Delphine Buysse (Tanzania/Belgium)
Rehema Chachage (Tanzania)
Cloud Chatanda (Tanzania)
Eneida Sanches (Brazil)
Jan Van Esch (Tanzania/Netherlands)
Aika Kirei (Tanzania)
Vita Malulu (Tanzania)
Gadi Ramadhani (Tanzania)
On view:
February 7 - March 7, 2015
In beauty salons and
barbershops of the Msasani area (Makangira street near Edo Chips), Dar es
Salaam, Tanzania
Synopsis:
Beauty Salons and the Beast will
introduce the Tanzanian public to new and experimental art and attempt to
increase public interest and dialogue in the happenings and role of the visual
arts in Tanzania. The project carries the theme of ‘multiple-choice’ and will
feature artworks and interventions from local Tanzanian and international
artists.
Beauty Salons and the Beast is
interested in the public sphere and in questioning the role of artists in
society by using artistic media and creative expression to engage with
communities to communicate, explore and articulate issues of local
significance. It employs the ‘if they don't follow the art, we will bring the
art to them’ module by ‘infecting the city’ with activities like public
performances, interventions and public discussion as a way of ‘bringing art’ to
the community, and as a dialogue starter.
The launch for the project
will be on 7th February 2015 at 14.00hrs and will feature exhibited
works of art in a total of 4 small and large beauty salons and barbershops
located in Makangira Street (Also known as Msasani street near Edo Chips) in
Dar es Salaam. The launch will feature entertainment, and speeches from the
organizing team, the artists as well as the sponsors for the project; apexart
an organization based in New York, USA.
Beauty Salons and the Beast is
organized by Rehema Chachage and Jan van Esch
COMMENTS