KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, PROFESA MAGHEMBE ALIKUWA MGENI RASMI

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR Wiki hii jijini Dar es Salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maj...

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR

Wiki hii jijini Dar es Salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maji kutoka kila kona ya nchi hii. Kubwa lililofanyiwa kazi na wataalam hao wa maji ni kujulishwa teknolojia mpya ya mabomba iliyokuwa inatambulishwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mambomba ya Borouge kutoka Falme za Kiarabu. 

Borouge ilileta wataalam wanne ambao ni Mario Andrade, Farraj Tashman, Andrew Wedgner na Reda Ashkar. Walionufaika na mafunzo hayo ni waliotoka Mamlaka za Maji mijini na vijiji, Wahandisi, Washauri katika fani zote za maji, ujenzi na gesi. 

Pia washiriki walifahamishwa kuwa sasa lile tatizo la mabomba ya matumizi yote yamefika mwisho kwani kiwanda cha pipe industries cha vingunguti mjini Dar es Salaam kitakidhi mahitaji ya nchi nzima na kuwa na ziada ya kuuza nje kwa amabomba ya aina zote kama vile hdpe, pvc, grp na mabomba chuma kwa upenyo wa 60mm mpaka zaidi ya 3,200mm. 

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe ambaye alionyeshwa kufurahishwa kwake na uwepo wa kiwanda kama hicho ambacho kinamilikiwa na wazawa kinahesabika kama kikubwa kuliko vyote afrika mashariki na kati pia cha aina yake kwa kuweza kuwa na uzalishaji wa mabomba aina yote katika kiwanda kimoja na chenye uwezo wa kuajiri watu 500.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akikagua bidhaa za mabomba yanayozalishwa na kiwanda cha Pipe Industries cha mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la wataaalam wa maji lilifanyika hivi karibuni. wa pili kushoto ni Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda hicho Bwana Nassor Ally Seif.
Mwekezaji mzawa wa Kiwanda cha Pipe Industries, Nassor Seif (kushoto) akimsikiliza Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akimweleza jambo kuhusiana na mabomba yanayozalishwa na pipe industries wakati akikagua maonyesho ya kiwanda hicho katika kongamano la maji lilofanyika mjini Dar es Salaam.
Waziri Maghembe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano hilo.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (wa pili kutoka kushoto) akifurahia jambo na wamiliki wa pipe Industries Nassor Seif (kushoto) na Seif Seif  (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano la maji. Kulia ni Esther Baruti Kroll, Mwakilishi Mkazi wa kampuni ya saruji ya Dangote Industries.
Wataalam vijana wa tanzania ni miongoni mwa washiriki na wawezeshaji wa kongamano la maji. Kushoto ni Moses Nkanda bingwa katika mambo ya mabomba ya gesi na Mtaalam Mshauri, Subiro Mwapinga.
Mtoa mada katika Kongamano la Teknolojia ya Maji kutoka Kampuni ya Borouge, Mario Andrade akitoa maelezo kwa washiriki wa kongamano la maji juu ya borouge na uwezo wake katikasekta ya mabomba.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano.
Mkurugenzi wa Superdol, Jamal Bayser (kulia) na Mkurugenzi wa Reni International, Dipak Vassa.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Mabomba cha Pipe Industries, Sebastian Kyoni (kulia) akiwa na wataalam wenzake wakishiriki katika kongamano la maji jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la maji.
Meneja wa Super Star Forwarders, Fulgence Bube (wa pili kulia) akielezea jambo kwa washiriki wenzake wa kongamano la maji. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa Superdol Jamal Bayser.
Bwana Andrew Wedgner wa Kampuni ya Borouge ya falme za kiarabu akitoa utalaam wake juu ya mabomba ya pe 100 wakayi wa kongamano la maji lilokuwa linafanyika mjini dar es salaam. kushoto ni bwana reda ashkar ambaye amebobea katika uunganishaji wa mabomba ya hdpe na ufundishaji wa teknolojia hiyo btoka kampuni ya borouge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Pipe Industries Bwana Seif Ally Seif akitoa maelezo ya kiwanda chake katika kongamano la maji lilofanyika jijini Dar es Salaam

COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, PROFESA MAGHEMBE ALIKUWA MGENI RASMI
KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, PROFESA MAGHEMBE ALIKUWA MGENI RASMI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgs0wXbA_RblG1kKsgmb0wA_e9NRPywBPRlYIZnuYMvszAs9h4Vi3M3FfmVxySKrfQ54mimSa2eFYm-rF2B4FA2v72GhWc1UFtjoh-89fZDhDCJIRWieJtGlgwkxF14MsfU0hNUresd-56q/s1600/DSC_8953.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgs0wXbA_RblG1kKsgmb0wA_e9NRPywBPRlYIZnuYMvszAs9h4Vi3M3FfmVxySKrfQ54mimSa2eFYm-rF2B4FA2v72GhWc1UFtjoh-89fZDhDCJIRWieJtGlgwkxF14MsfU0hNUresd-56q/s72-c/DSC_8953.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2014/06/kongamano-la-maji-lafanyika-jijini-dar.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/06/kongamano-la-maji-lafanyika-jijini-dar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy