YAHAYA WA JAY DEE WAMPAMBA LULU KWENYE MY FOOLISH AGE

MSANII wa Filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' ameonyesha kipaji chake kwa kuimba vyema wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muzik...



MSANII wa Filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' ameonyesha kipaji chake kwa kuimba vyema wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee, na kutunzwa mijihela wakati akiimba wimbo huo na Jide kwenye uzinduzi wa Video yake mpya na ya kwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE Agosti 30 2013.

Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyoonyesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wapenzi na mashabiki wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao ambapo  alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Lulu alianza kwa kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, na kuwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alitamka kuwa kweli muziki unalipa.
“Jamanieee kumbe muziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona mijihela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba muziki”, alisema Lulu, huku akishangiliwa na mashabiki wake.

Uzinduzi wa filamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.






 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City. (Picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog)
 Lulu Michael akizungumza machache mara baada ya Move yake kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 
 
 Jide akikamua jukwaani... 
 
 
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
 .... Walitunzana tu kivyao vyao...
 

 noti alizo tuzwa Jide...
 Rich Rich akimwaga noti
 
 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
 
Wakongwe wa Bongo Muvi wakifurahia jambo.
 
 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 
 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: YAHAYA WA JAY DEE WAMPAMBA LULU KWENYE MY FOOLISH AGE
YAHAYA WA JAY DEE WAMPAMBA LULU KWENYE MY FOOLISH AGE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJucWQxfNmJ4PEOsnFOhb7FhMIP0k3BUWv4XF0Y-nwRtMsZLvenwtSxEC8kFUmnvUAPEiZgo2cGR-BcbS-x114YbvohBK5ZGpJmwlPwpPNgW6fr64nqz8anEThhTSOgibiNf9-ZbQXZhKQ/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJucWQxfNmJ4PEOsnFOhb7FhMIP0k3BUWv4XF0Y-nwRtMsZLvenwtSxEC8kFUmnvUAPEiZgo2cGR-BcbS-x114YbvohBK5ZGpJmwlPwpPNgW6fr64nqz8anEThhTSOgibiNf9-ZbQXZhKQ/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2013/08/yahaya-wa-jay-dee-wampamba-lulu-kwenye.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/08/yahaya-wa-jay-dee-wampamba-lulu-kwenye.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy