MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, MHE. ANNA MNGWIRA, AZINDUA MPANGO WA UHIFADHI MAZINGIRA WILAYANI SAME.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mngwira, (watatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe.Rosemary Sitaki, na viongozi wengine wakishiriki...







Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mngwira, (watatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe.Rosemary Sitaki, na viongozi wengine wakishiriki kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mpango wa mazingira NA kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Same.
NA MWANDISHI WETU.SAME

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mngwira, amezindua mpango wa uhifadhi mazingira wilayani Same, na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyohudhuriwa na zaidi wa watu 10,000.
Katika hafla hiyo iliyofana ambapo Wanasame walionyesha umoja na ushirikiano wa pekee kuanzia wananchi, viongozi wa vijiji hadi Taifa, taasisi za dini, NGOs, Taasisi za serikali na binafsi,
Wote walionekana kutoka na dhamira moja ya kuyabadili mazingira ya Same kwa dhati.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mngwira aliyekuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo akimuwakilisha Waziri wa Muungano na Mazingira; Alitumia nafasi hiyo kutoa maagizo 6 muhimu kwa Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Ikiwa ni pamoja na kuupamba Mkoa kwa kupanda miti kwenye barabara kuu zoote kuanzia Same mpaka Hai.
Pia DC wa Same Mh. Rosemary Sitaki aliwakumbusha wananchi wa Same kuwa, hakuna litakaloshindikana wakiamu " Dhamira yashinda vikwazo, hivyo tuamue kuyabadili mazingira yetu" Aliwashukuru wote walioshiriki na kuwa Historia ya Same haitawasahau.
Shirika la Floresta lilikuwa ni mdau mkubwa katika kufanikisha sherehe hiyo. Lina vikundi 390 vyenye wanachama 8700 kwa Mkoa mzima. Na linafanya kazi kubwa sana katika mazingira likiongozwa na Mkurugenzi Richard Mhina.


Mhe. Sitaki akipanda mche wa mti.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mngwira, DC wa Same Mhe. Rosemary Sitaki na viongozi wengine wakisakata dansi ikiwa ni kushajihisha uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mngwira, akihutubia wakati wa hafla hiyo.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mngwira, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, MHE. ANNA MNGWIRA, AZINDUA MPANGO WA UHIFADHI MAZINGIRA WILAYANI SAME.
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, MHE. ANNA MNGWIRA, AZINDUA MPANGO WA UHIFADHI MAZINGIRA WILAYANI SAME.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiEQwQIsqrc0pxkDf72juQp28MgrG1L9Hen80Qfl_ZFz8-Uh8G7U7b08vRpzFtXd-0TjN0VxJs-bla5nuaxITMv779WKGyzHsnqJFQZ18Hh3RVYiKRMVrezqejonm7nfaXmDCMVZ064WvX/s640/untitled.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiEQwQIsqrc0pxkDf72juQp28MgrG1L9Hen80Qfl_ZFz8-Uh8G7U7b08vRpzFtXd-0TjN0VxJs-bla5nuaxITMv779WKGyzHsnqJFQZ18Hh3RVYiKRMVrezqejonm7nfaXmDCMVZ064WvX/s72-c/untitled.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/mkuu-wa-mkoa-wa-kilimanjaro-mhe-anna.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/mkuu-wa-mkoa-wa-kilimanjaro-mhe-anna.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy