Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tan...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kukabidhi matembezi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi mapema leo asubuhi mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.Mbali ya Makamu wa Rais kuunga mkono tukio hilo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, Naibu waziri wa Afya. Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla na wengineo sambamba na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza mazoezi ya kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

Wananchi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji wa Dodoma wakishiriki mazoezi mapema leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma. (Picha VPO)
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Na. Lilian Lundo-Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi
kufanya mazoezi na kupumzika.
kufanya mazoezi na kupumzika.
Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.
"Ni muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alisema Mhe. Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema kwamba, muitikio wa ufanyaji mazoezi wa viungo ni mkubwa, ambapo watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.
Aidha, amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpuzika.
Ameongeza kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya yao na kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.
Vile vile amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kuhamasisha mazoezi ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya kila mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.
Aliendelea kwa kusema kuwa, mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na saratani.
Aidha amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo wawahamasishe wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kulinda afya zao.
Uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzia viwanja vya Bunge na baadaye
alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wananchi wa Mkoa huo.
COMMENTS