Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya tuzo ya kima...
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) juu ya tuzo ya kimataifa ya viwango iliyotolewa
na International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM)
kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) vitabu vya mtaala mpya wa mafunzo ulioanza na Bodi ya
wataalamu ya manunuzi na Ugavi (PSPTB) Disemba mwaka 2015. Kulia ni
mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) tuzo ya viwango vya kimataifa kutoka International
Federation of Purchasing and Supply Manangement (IFPSM) iliyotolewa kwa
kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa Bodi ya wataalamu wa
manunuzi na ugavi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Hassan Silayo MAELEZO).
Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Bodi
ya wataalam wa manunuzi na ugavi (PSPTB) imetunukiwa tuzo ya viwango vya
kitaalamu vya kimataifa na International Federation of Purchasing and
Supply Manangement(IFPSM) na kutambulika rasmi kimataifa kwa kuwa na
vigezo vya utoaji huduma katika viwango vya kimataifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dare s Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa
PSPTB Bw. Clemence Tesha amesema tuzo hiyo imetolewa kwa PSPTB mwezi
Februari mwaka 2016 na kuifanya PSPTB kuwa bodi ya kwanza barani Afrika
kupata tuzo hiyo ya viwango vya kimataifa kutoka IFPSM.
“Upatikanaji
wa tuzo hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya watendaji na mimi
mwenyewe kama Mkurugenzi Mtendaji wa bodi katika kuiendesha bodi hiyo
kufanikisha malengo na mipango yake katika utendaji kazi.
Bw
Tesha ameeleza kuwa mara baada ya PSPTB kupata tuzo hiyo wamepata
pongezi kutoka Rais wa IFPSM Dkt Paul Davi kwa niaba ya Bodi ya
wataalamu wa viwango vya kimataifa kwa kazi kubwa walioifanya na kuwa
taasisi ya kwanza Barani Afrika kufikia kiwango cha kutambulika
kimataifa kwenye taaluma hiyo.
Kabla
ya kupata tuzo hiyo, PSPTB ilikuwa mwanachama muhusishwa wa IFPSM tangu
mwaka 2015 lakini kutokana na utendaji wa kazi wake, Bodi ya viwango ya
kimataifa ikawatunuku tuzo ya kuwa na viwango vya kimataifa katika
utoaji wa taaluma hiyo Barani Afrika kwa ujumla.
Aidha ,
PSPTB imezindua mtaala mpya wa mafunzo tangu Desemba mwaka 2015 na
mtaala huo kwa sasa unaendelea kufundishwa katika vituo mbalimbali vya
maandalizi ya mitihani ya Bodi ambapo mtihani wa kwanza chini ya mtaala
mpya utafanyika November 2016.
Umuhimu
wa mtaala huo ni pamoja na utaratibu wa kuanzisha masomo ya usimamizi
wa manunuzi wa umma kuanzia ngazi za chini hadi juu na pia utaratibu huu
utawataka watahiniwa kufaulu ngazi yoyote ya mtihani ndani ya miezi 24
toka kufanyika kwa mtihani husika kwa mara ya kwanza.
Katika
kuzingatia utoaji wa taaluma ya manunuzi na ugavi nchini Bodi ya
wataalamu wa manunuzi na ugavi itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kusaidiana na kupambana na
changamoto zilizopo katika kupeleka mbele gurudumu la taaluma hiyo.
COMMENTS