‘ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’ WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekele...
‘ASILIMIA 10 YA
WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji
ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Taarifa
zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa
nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi
wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika
na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri
Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka
na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi,
misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne,
Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano
cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya
uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia
alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua
mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na
Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo
ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake
na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye
Mweyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Profesa Omari Issa alisema katika dunia ya sasa
imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au
kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa
kuwaunganisha na masoko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016.
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016.
|
Add caption |
COMMENTS