MWANAFUNZI ALIYECHOMWA MOTO AKIDHANIWA MWIZI AFARIKI DUNIA, KUMRADHI PICHA INATISHA. Mwanafunzi Daniel Lema aliyejeruhiwa kwa moto ...
MWANAFUNZI ALIYECHOMWA MOTO AKIDHANIWA MWIZI AFARIKI DUNIA, KUMRADHI PICHA INATISHA.
![]() |
Mwanafunzi Daniel Lema aliyejeruhiwa kwa moto |
![]() |
Kijana Daniel Lema kabla ya kifo chake |
![]() |
DANIEL Lema kabla ya kujerihiwa na kifo chake |
Mwanafunzi
huyu Daniel Lema alikuwa akisoma mwaka wa nne, kozi ya sheria katika chuo
kikuu kishiriki cha Mt. Augustino cha Ruaha Iringa (Ruaha University College
maarufu kama RUCO).
Mwanafunzi
huyo alichomwa moto wiki iliyopita akihusishwa na tuhuma za wizi.
Baada
ya kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa wiki moja sasa, mwanafunzi
huyo ameaga dunia majira ya saa nane mchana.
Taratibu
za kuaga mwili wake zinaendelea kufanywa na uongozi wa chuo hicho, ndugu na
wanafunzi wenzake.
Taarifa
za awali zinaonesha kwamba mwili wake utaagwa kesho kuanzia saa moja asubuhi
kabla ya kusafirishwa kupelekwa kwao mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Mazishi ya
kijana huyo yanatarajia kufanyika jumatano ya wiki hii.
Juni 24, mwaka huu Daniel Lema alikutwa na mkasa wa kukamatwa na kuchomwa moto wakati akitoka kuangalia fainali za kombe la dunia katika moja ya Bar za mjini Iringa.
Akiwa
amelewa aliingia katika moja ya migahawa ya mjini hapa akitafuta chakula,
ilikuwa majira ya saa tano mwanafunzi huyo
aliingia kwenye mgahawa ambao biashara hiyo ilikua imefungwa.
Binti aliyekuwepo katika mgahawa huo alianza kupiga kelele
akidhani kavamiwa na mwizi. Mlinzi wa eneo hilo (mmasai) alimvaa kijana huyo na
kumshambulia.
Baada ya
tukio hilo taarifa zinasema walitokea watu wawili waliojitambulisha kuwa ni
askari; askari hao walizuia watu waliozidi kujitokeza katika eneo hilo
kuendelea kumpiga kijana huyo.
Wakiwa
njiani, wananchi hao waliokuwa wakifuatilia kama atafikishwa kituo cha Polisi
waliona wanachalewa na kuamua kuchukua sheria mkononi kwa kuendelea kumpiga
kabla ya kumchoma moto.
COMMENTS