Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Pascal Shelutete akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Mwanasayansi ...
Meneja Mawasiliano wa Shirika la
Hifadhi za Taifa TANAPA, Pascal Shelutete akizungumza jambo
wakati wa mkutano wa Mwanasayansi na Mtafiti mahiri wa Sokwe Duniani,
Dkt. Jane Goodall (wa pili kushoto) na waandishi wa habari kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanapa, liko mbioni
kumpatia tuzo Mwanasayansi na mtafiti mashuhuri Duniani, Dkt. Jane Goodall.
Hayo yalisemwa na Afisa Uhusiano wa TANAPA,
Pascal Shelutete wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Hifadhi ya Taifa
Gombe iliyoko mkoani Kigoma wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari nchini.
“Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa, linatambua
mchango mkubwa wa Mwanasayansi na mtafiti maarufu wa Sokwe Dunaini, Dkt. Jane Goodall,
katika jitihada za shirika kuhifadhi wanyama na mazingira yanayowazunguka.”
Alisema Shelutete wakati wa hafla hiyo fupi iliyowakutanisha waandishi na
mtafiti huyo mwenyeumri wa miaka 82.
Dkt.Goodall mzaliwa wa Uingerezaambaye amefanya
tafiti kwa muda mrefu nchiniTanzania, takribanmiaka 50, ametoa mchango mkubwa
katikakukuza utalii wa Tanzanianje yanchi kutokana na utafiti wakewa Sokwe,
kwenye Hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe. Kutokana na kufanyautafiti wa Sokwe kwa
muda mrefu kwenye Hifadhi hiyo, Dkt. Goodallana uwezomkubwa wa kuwasiliana na
wanyama hao kwa milio tofauti tofauti.
Dkt. Jane Goodall, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Hifadhi ya Taifa ya Gombe mkoani Kigoma
Dkt. Goodall, akiwa na maafisa wa TANAPA, pamoja na kundi lawaandishi wa habari huko Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Dkt. Goodall akisalimiana na Pascal Shelutete, Meenja Mawasiliano wa TANAPA, kwenye Hifadghi ya Taifa ya Gombe, mkoani Kigoma
Dkt. Goodall akionyesha mapenzi makubwana Sokwe, kiasi kwamba wanyama hao wamekuwa rafiki yao kubwa
Dkt. Goodall aliipenda Tanzania tangu akiwa msichana "mbichi"
Dkt. Goodall akiwa na Sokwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Gombe, mkoani Kigoma
COMMENTS