JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA

Msanii Juma Nature 'Kiroboto' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamas...










Msanii Juma Nature 'Kiroboto' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini  pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said Christopher 'Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii  Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri 'Msagasumu' na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix 'Fredwayne' Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher 'Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

............................................................................................................
                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                           
KOMAA CONCERT

Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya
msanii JUMA NATURE  maarufu kama kiroboto pamoja na hitimisho la
sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA
CONCERT
kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi  jumamosi hii ya  tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar
Alive –Mbagala,  kuanzia saa kumi na
mbili jioni.

Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana
na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Aidha, mashabiki watapata burudani kutoka kwa
kiroboto  ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na  Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.

Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm
Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.

Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji
kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya.

Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza itaendelea
kufanya hivyo kwa wasanii wengine
kwakuwa kwetu sisi
tunaamini Muziki unaongea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

IMETOLEWA NA, DENIS SSEBO,
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM.



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA
JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL8_p8H67xpfWBT4D0EUqtjEptEkBwUqS2gaIdxHDtYg5OmnqU_Xg_3VdYAeo8Xfj82_uqn7witFECbBOTjTAvO1hu96LipoIoJ1AFthfMtniSbGCW6-zN7OgPmTcaoVMwHO3-NgPD_Vg/s640/2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL8_p8H67xpfWBT4D0EUqtjEptEkBwUqS2gaIdxHDtYg5OmnqU_Xg_3VdYAeo8Xfj82_uqn7witFECbBOTjTAvO1hu96LipoIoJ1AFthfMtniSbGCW6-zN7OgPmTcaoVMwHO3-NgPD_Vg/s72-c/2.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/juma-nature-na-wenzake-kuiteka-dar-es.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/juma-nature-na-wenzake-kuiteka-dar-es.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy