MUDA WA KUSHUGHULIKIA MIZIGO MPAKANI RUSUMO WAPUNGUA

Na Veronica Kazimoto Zanzibar 29 Mei, 2018. Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia Mamlaka zake za Mapato zimefanikiwa kupungu...


Na Veronica Kazimoto
Zanzibar
29 Mei, 2018.

Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia Mamlaka zake za Mapato zimefanikiwa kupunguza muda wa kushughulikia mizigo mpakani Rusumo mkoani Kagera kwa asilimia 73.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Zanzibar.
Kichere amesema kuwa, baadhi ya mafanikio muhimu ya  mradi huu ni pamoja na uendeshaji wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani kwenye mipaka ya Rusumo na Namanga na maendeleo ya uwezo wa utendaji kazi wa maofisa wa forodha na mawakala.
"Mafanikio ya mradi huu yanaonekana wazi, kwa mfano tukichukulia mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, muda wa kushughulikia mizigo mpakani hapo umepungua kwa asilimia 73% yaani kutoka masaa manane na dakika 42 hadi kufikia masaa mawili na dakika 20 tu," alisema Kichere.
Mradi huu wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ni wa miaka mitatu na nusu ambao unafadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na ulizinduliwa rasmi mwezi Desemba, 2017.
Mradi huu unatekelezwa  na Mamlaka tano za Mapato  za nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika leo Zanzibar. Kushoto ni Mhe. Audace Niyonzima wa Mamlaka ya Mapato Burundi na kulia ni Bw. Toshio Nagase Mwakilishi Mkazi wa JICA.



Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna Wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki na wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MUDA WA KUSHUGHULIKIA MIZIGO MPAKANI RUSUMO WAPUNGUA
MUDA WA KUSHUGHULIKIA MIZIGO MPAKANI RUSUMO WAPUNGUA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEherYhdHwt_C2zNoJQ236G8rjVLCERhw7mGoBxPSNTCNpM0BYd9hDrSqnDjVoic_4dUMF1pP51wiHlTPVNAV9yipBGPoH5HPbOC24kMCqWYi3Dzm-myZHe_7DvUosGnxlq8kSNHreccQhg/s640/PICHA+NAMBA+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEherYhdHwt_C2zNoJQ236G8rjVLCERhw7mGoBxPSNTCNpM0BYd9hDrSqnDjVoic_4dUMF1pP51wiHlTPVNAV9yipBGPoH5HPbOC24kMCqWYi3Dzm-myZHe_7DvUosGnxlq8kSNHreccQhg/s72-c/PICHA+NAMBA+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/muda-wa-kushughulikia-mizigo-mpakani.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/muda-wa-kushughulikia-mizigo-mpakani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy