Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celina Ompeshi Komban...
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celina Ompeshi Kombani umewasili nchini leo kutokea Nchini India alikofia na kupokelewa na watu mbalimbali wakiwepo Viongozi wa Serikali,
Ndugu jamaa na marafiki.
|
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashillilah akitangaza utaratibu wa kuuhufadhi mwili katika hospitali ya Lugalo baada ya kuwasili uwanja wa JNIA leo. |
|
Mme wa Waziri Kombani, Bwana Salehe Konglani akisalimiana na Naizbu Waziri wa Sayansi na Tekinoloia, Mh. Januari Makamba pamoja na viongozi wengine waliofika kuwafariji wafiwa na kuupokea mwili wa marehemu. Anayemtambulisha ni Waziri wa Afya na Usatwi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. |
|
Mme wa Waziri Kombani, Bwana Salehe Konglani akifajiana na wafiwa wenzake. |
|
Mme wa Waziri Kombani, Bwana Salehe Konglani alipowasili katika uwanja wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutokea India na mwili wa mwenza wake. |
|
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Katibu mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipowasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuupokea mwili wa Waziri Kombani. |
|
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifajiana na Spika wa bunge Mh. Anne Makinda alipowasili uwanja wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuupokea mwili wa Waziri Kombani. |
COMMENTS