Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia waumini wa Dini ya Kikristo wakati wa ghafla y...
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia waumini wa Dini ya Kikristo
wakati wa ghafla ya kuwekwa wakfu Askofu mpya
wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel
Joseph Makala na kuzinduliwa kwa Dayosisi hiyo mpya ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria iliyofanyika jana katika kanisa la Ebeneza Shinyanga mjini. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Emannuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu na kuzinduliwa
kwa Dayosisi hiyo katika Kanisa la Ebeneza Shinyanga mjini Mei
5, 2013. Katikati ni Askofu Mkuu KKKT Tanzania, Dk. Alex Malasusa. |
|
Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria
Mchungaji Emannuel Joseph Makala akiwa na wazazi na ndugu wa karibu baada ya kuwekwa wakfu. |
|
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu. |
|
Makamu wa Rais wa
Tanzania Dt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na
Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria, Emmanuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu. (Picha na OMR) |
COMMENTS