Combination ya Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco, A.K.A Adebayo, na mshambualiaji wa Kimataifa kutoka Uganda, Emmanuel Anold...
Combination ya Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco, A.K.A Adebayo, na mshambualiaji wa Kimataifa kutoka Uganda, Emmanuel Anold Okwi, inazidi kuimarika, baada ya Januari 28, 2018 kila mmoja akipachika mabao mawili wakati Simba ikiibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye pambano la kufunga raundi ya kwanza ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
John Bocco ndiye alikuwa wakwanza kufunga bao baada ya kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Shizah Kicvhuya kutoka Magharibi mwa uwanja wa Taifa goli la Kusini, kunako dakika ya 16 na dakika 10 baadaye yaani dakika ya 26 John Bocco tena alifunga bao la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Said Ndemla, kutoka upande wa Mashariki, goli la kusini mwa uwanja wa Taifa.
Timu zilienda mapumzikoni Simba ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Combination ya Bocco na Okwi, pia imeonekana kuleta manufaa, kwani wamekuwa wakielewana vilivyo uwanjani na hivyo kuwapa chaguo gumu walinzi wa timu pinzani wasijue ni yupi wamkabe sana.
Safari hii bao la tatu la Simba, lilifungwa na Emmanuel Okwi, kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na John Bocco, ambaye alikokota mpira kutoka mita chache kwenye mduara wa uwanja, na kukipita "kijiji" cha walinzi wa Majimaji, kabla ya kumimina krosi ya chini chini na kumkuta Okwi upande wa Mashariki mwa uwanja wa Taifa ambapo kabla ya kupachika bao hilo "alimfinya: mlinzi wa Majimaji na kufumua shuti kwa kutumia mguu wake wa kushoto na kupachika bao.
Bao la nne la Simba lilifungwa tena na Okwi, kufuatia kona ya Shizah Kichuya, ambayo ilikuja chini chini wakati mlinzi wa Majimaji akijaribu kuokoa mpira ulipaa juu na kuja katikati ya goli ambapo Okwi alijitwisha kwa kichwa na kipa kuokoa lakini Okwi a,ifanikiwa tena kuunasa mpira huo na kuutumbukiza kimiani.
Simba sasa wamefikisha pointi 35 na magoli 35 wakiwa mbele ya Azam FC na Yanga. Msimamo wa VPL hadi sasa ambapo raundi ya kwanza imemalizika ni kama ulivyo hapo chini.



COMMENTS