MAKAMU WA RAIS, MHE SAMIA SULUHU AHAMIA DODOMA RASMI

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA 15/12/2017 Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia ras...



Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA
15/12/2017
Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.
 Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.
“Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia
Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo  wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .
“Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.
“Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na  kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.
Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.
“Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.
Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.
Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Add caption

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma ya Kigogo pamoja na wasanii wa kikundi cha Hiari ya Moyo Mwinamila wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitamka kukubali karibu ya kuhamia Dodoma akishuhudiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya Kilimani, mjini Dodoma. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)






COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS, MHE SAMIA SULUHU AHAMIA DODOMA RASMI
MAKAMU WA RAIS, MHE SAMIA SULUHU AHAMIA DODOMA RASMI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV3MhrTvg0C6-gQSNZbzNYRiHRdNRZzh1xL3RkWyyy67Oo-v6HgwpCOWXXTSsVojiBdfixh7LR5DuDhSkixKkPBDrdRAQqIwhVN0se7ts2pXn0S2QADFbVk8oMHZ_OrWbpH55mrT18mUo/s640/6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV3MhrTvg0C6-gQSNZbzNYRiHRdNRZzh1xL3RkWyyy67Oo-v6HgwpCOWXXTSsVojiBdfixh7LR5DuDhSkixKkPBDrdRAQqIwhVN0se7ts2pXn0S2QADFbVk8oMHZ_OrWbpH55mrT18mUo/s72-c/6.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-ahamia.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-ahamia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy