Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi(kulia), akimkabidhi moja ya meza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu...
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi(kulia), akimkabidhi moja
ya meza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.(Mwenye suti nyeusi),
kwa ajili ya shule ya sekondari Ikoma iliyoko wilayani huko. TPB imetoa
madawati 50, ikiwa ni pamoja na viti na meza kama msaada wa benki
kusaidia sekta ya elimu nchini. Msaada huo una thamani ya shilingi
milioni 4.
Mkuu wa wilaya. Nurdin Babu, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba
Moshingi, akikaribushwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu
kwenye shule ya sekondari Ikoma, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa
madawati.
TPB yachangia madawati Serengeti
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imetoa mchango wa madawati na viti 50 vyote
vikiwa na thamani ya shilingi Milioni Nane kwa Shule ya Sekondari ya
Ikoma, iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara. Mchango huo wa madawati
ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na Afisa
Mtendaji Mkuu wa (TPB) Sabasaba Moshingi, kwenye hafla fupi iliyofanyika
shuleni hapo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki yake
imeamua kutoa viti pamoja na madawati hayo ili kuhakikisha kuwa
wanafunzi wote watakaoanza kutumia shule hiyo hapo mwakani watakaa
kwenye mazingira mazuri yanayofaa. Pia alitoa pongezi nyingi kwa uongozi
wa Kijiji hicho cha Ikoma kwa bidii zao zilizohakikisha kuwa
wanakamilisha ujenzi wa madarasa pamoja na maabara, tayari kwa kupokea
wanafunzi mwaka ujao. Aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi
huo ili kuweza kukabiliana na changamoto nyingine kama vile uhaba wa
nyumba za waalimu na mabweni zinazoendelea kuikabili shule hiyo.
Naye
mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo Mhe. Nurdin Babu aliishukuru Benki ya
Posta kwa msaada huo uliofika wakati muafaka, ambapo shule hiyo
inajiandaa kupokea wanafunzi wapya. Alisema kuwa ni wajibu wa kila
Mtanzania mwenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa anatoa kipaumbele kwa
sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wetu kupata elimu kwenye mazingira
mazuri. Alitoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea
kuchangia sekta ya elimu hususan shule hiyo, ili waweze kutatua changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo.
COMMENTS