WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

    ‘ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’ WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekele...

 

 

‘ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 

“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.

Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.

Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Profesa Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016. 


Add caption


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola  (wa pili kulia) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa  Wadau wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)








COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiydQBcnqu1wt630GVyOUT-L7XhDw1YTpLF0MRT2hPc8Ld2lVts9BKbbcdr25rE6zYOil0X1gEqTroA0razsToMF3gQDuZqjq5GLEpPYfVLUl42ZcGlsPASaVThK3ghf0qcmF_yECt4Uup2/s640/IMGS3539.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiydQBcnqu1wt630GVyOUT-L7XhDw1YTpLF0MRT2hPc8Ld2lVts9BKbbcdr25rE6zYOil0X1gEqTroA0razsToMF3gQDuZqjq5GLEpPYfVLUl42ZcGlsPASaVThK3ghf0qcmF_yECt4Uup2/s72-c/IMGS3539.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/waziri-mkuu-majaliwa-afungua-mkutano-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/waziri-mkuu-majaliwa-afungua-mkutano-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy