VIDEO MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU DKT. LAISER NA UZINDUZI WA DAYOSISI YA KKKT

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikal...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.
Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu  na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora.
Makamu wa Rais amesema hivi karibuni Serikali imepitisha mabadiliko na mpango mpya wa uwekezaji Tanzania.
Makamu wa Rais amesema kuwa kudumisha Amani na usalama ni jukumu la wote “ Endeleeni kuhubiri Amani na kwa upande wa Serikali niwahakikishie Watanzania Wote kwamba Amani na Usalama ni kipaumbele chetu hatuta vumilia kumstahimilia mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kuharibu Amani ya Tanzania hatutamvumilia tutamshughulikia ipasavyo”
Makamu wa Rais amesema “Tukosoeni pale tunapokosea nasi tunawaahidi tutarekebisha na twende mbele kwani Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza nikuonyesha njia na katika kuonyesha njia lazima ukubali kukosolewa nasi tunakubali kukosolewa hilo nalo ni jukumu la utumishi wa kiroho kwa hiyo endeleeni kutukosoa kwa ile lugha ambayo tutafahamiana”
Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Taasisi za dini katika masuala ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii.
Makamu wa Rais amelishukuru na kulipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa mchango wake mkubwa unatoa katika nchi yetu hususani katika Nyanja za Elimu, Huduma za Afya na Maji.
Nae Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo alisema kuwa wameona jitihada za Mheshimiwa za Rais na wataendelea kumuunga mkono na wapo pamoja kushirikiana na Serikali kwa nia njema kabisa.












COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIDEO MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU DKT. LAISER NA UZINDUZI WA DAYOSISI YA KKKT
VIDEO MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU DKT. LAISER NA UZINDUZI WA DAYOSISI YA KKKT
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/video-makamu-wa-rais-ahudhuria-kuwekwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/video-makamu-wa-rais-ahudhuria-kuwekwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy