Mei 17, 2018 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara, kwen...
Mei 17, 2018 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara, kwenye ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Sambamba na uzinduzi huo, akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mdunku na Lesoit vilivyopo wilayani humo, Naibu Waziri Mgalu alielekeza kampuni inayofanya kazi hiyo ya Angelique International Limited kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya umeme huku ikihakikisha taasisi zote kama vituo vya afya, shule na zahanati zinapata umeme wa uhakika.
Aliwataka wananchi kujiandaa na fursa mbalimbali za uwekezaji katika viwanda vidogo na kilimo kutokana na matumizi ya nishati ya umeme ili kujiletea maendeleo. Katika hatua nyingine, Mgalu aliwataka wananchi kujiepusha na matapeli na vishoka na kusisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa matapeli.
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa na kulia ni Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian.
|
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa (kushoto) Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian (kulia) pamoja na wananchi wengine wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara.
|
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa.
|
|
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara wakisikiliza hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo
|
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akielezea mikakati ya Wizara yake kwenye usambazaji wa umeme vijijini |
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Lesoit kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
|
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akitoa ufafanuzi kuhusu miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na REA katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mdunku kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara. |
|
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akijibu kero mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi wa kijiji cha Kijungu kilichopo wilayani Kiteto mkoani Manyara. Wananchi hao walisimamisha msafara wake kwa ajili ya kuwasilisha kero mbalimbali ikiwamo kutounganishiwa huduma ya umeme kwa muda mrefu. |
COMMENTS