GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

 Wasamaria wema wakiwa wamewabeba watoto waliogongwa na gari la mizigo katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, eneo la Kituo ...

 Wasamaria wema wakiwa wamewabeba watoto waliogongwa na gari la mizigo katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, eneo la Kituo Kipya, Gongo la Mboto, Dar es Salaam leo.


Na Richard Mwaikenda, GOMS


WATOTO wawili wamegongwa na gari la mizigo  katika ajali iliyotokea mchana wa leo 

katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, Gongo la Mboto (Goms), Dar es Salaam.


Watoto  hao wawili ndugu wa kike na wa kiume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka minne na mitano walipatwa na mkasa huo muda mfupi baada ya mama yao kuwaacha pembezoni mwa barabara.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema ajali hiyo ilitokea wakati gari  gari namba T 324 PTM lililokuwa kwenye mwendo kasi kuikwepa bodaboda iliyokuwa iliyokatiza ghafla mbele yake, ndipo likapoteza mwelekeo na kuwagonga watoto hao.


Gari hilo ambalo dereva alikimbia baada ya ajali kuogopa kipigo, liliwagonga watoto hao na kuingia kwenye mtaro, lakini kama siyo mtaro lingeingia kwenye nyumba na kusababisha maafa zaidi.Mwendesha bodaboda naye alikimbia kuogopa kipigo.


Watu wengine wakiwemo waendesha bodaboda wanaoegesha kusubiri abiria katika kona hiyo ilipo transfoma, walinusurika kwani wengi wao hawakuwepo na baadhi yao walikimbia baada kuliona gari hilo limekosa mwelekeo.


Wanasema kuwa mama mzazi wa watoto hao ambaye hakuwa mbali sana na eneo la ajali aposikia mkasa huo hakuamini na kilichofuata aliishiwa nguvu na kuanguka chini.


Baadhi ya wasamaria wema waliharakisha kuwachukua watoto hao waliokuwa kwenye hali mbaya na kuwaingiza kwenye Bajaji tayari kuwakimbiza hospitali kwa matibabu. 


Ajabu iliyotokea ni kwamba baadhi ya waendesha Bajaji walikataa katakata kuwapeleka watoto hao Hospitali. Watoto waliojeruhiwa wakiwa chini baada ya kuwaokoa chini ya gari kwenye mtaro Watoto majeruhi wakiingwa kwenye moja ya bajaji kuwawahisha hospitali, lakini hata hivyo mwendesha bajaji hiyo alikataa kuwapeleka na kuwaamuru wawashushe. (IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203)

 Wakihamia kwenye moja ya Bajaji kuomba msaada huo

 Wakiwaingiza kwenye Bajaji ambayo walikubaliwa

 Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akilia kwa uchungu baada ya kuwaona watoto hao

 Wakiangalia ajali hiyo

 Gari hilo nusura liingie kwenye maduka yaliyopo eneo hilo, kilichozuia ni mtaro wa maji taka, Trafiki akiangalia ajali hiyo Breakdown ikiandaliwa kulivuta gari. Hata hivyo lilishindwa

Gari hilo likivutwa na gari la taka

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO
GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO
https://2.bp.blogspot.com/-_jCpis-dNQg/Wq0gR6M6xCI/AAAAAAABJM4/GGGxcpZRZS8urSZ4RHkMIuwtCldK2OYWACLcBGAs/s640/01.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-_jCpis-dNQg/Wq0gR6M6xCI/AAAAAAABJM4/GGGxcpZRZS8urSZ4RHkMIuwtCldK2OYWACLcBGAs/s72-c/01.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/gari-lagonga-watoto-kuikwepa-bodaboda.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/gari-lagonga-watoto-kuikwepa-bodaboda.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy