BENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA DHAMANA YA KAZI NA MIKOPO WAKANDARASI

Mkurugenzi wa benki ya CRDB, huduma kwa wateja wakubwa, Goodluck Nkini akizungumza kwenye semina kwa Wakandarasi iliyoandaliwa na benki ...


Mkurugenzi wa benki ya CRDB, huduma kwa wateja wakubwa, Goodluck Nkini akizungumza kwenye semina kwa Wakandarasi iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanroad pamoja na kampuni ya uuzaji mitambo ya Mantrac.
Semina hiyo ilifanyika jana Jijini Mwanza na kuwakutanisha Wahandisi na Wakandarasi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza.

Na Binagi Media Group
Benki ya
CRDB imewahakikishia Wakandarasi upatikanaji wa mikopo pamoja na dhamana ya
kazi, itakayowawezesha kuwa na vigezo vya kupata tenda na hatimaye kutimiza
vyema shughuli zao.

Mkurugenzi
wa CRDB mkoani Mwanza, Wambura Calystus alitoa ahadi hiyo jana kwenye semina
kwa wakandarasi wa barabara, iliyoandaliwa na beki hiyo kwa kushirikiana na wakala
wa barabara Tanroad mkoa wa Mwanza pamoja na kampuni ya uuzaji na ukodishaji wa
mitambo ya Mantrac.

“Miradi ya
ujenzi na miundombinu imekuwa mingi katika nchi yetu hivyo tumeona ni bora
benki yetu ya CRDB iweze kukaa na wakandarasi ili tuone namna bora ya kuwafikishia
huduma waweze kujenga miundombinu hiyo bila tatizo”. Alisema Calystus.

Naye Mkurugenzi
wa CRDB huduma kwa wateja wakubwa, Goodluck Nkini alisema ushirikiano baina ya
benki hiyo, Tanroad pamoja na kampuni ya Mantrac utawasaidia wakandarasi
hususani wadogo kupata mitambo bora ya kufanyia kazi na hivyo kutimiza vyema
majukumu yao.

“CRDB
itawezesha wakandarasi kupata mitambo na kuondoa kero iliyokuwepo awali ya
wakandarasi kukosa kazi kwa sababu ya kutokuwa na mitambo”. Alisema Meneja
Mauzo kutoka kampuni ya Mantrac Kanda ya Ziwa, Eutachius Katiti.

Awali Kaimu
Meneja wa Tanroad mkoani Mwanza, Joseph Mwami alikiri kwamba wakandarasi wengi walikuwa
wakikumbana na changamoto ya kupata kazi kutokana na kukosa dhamana ya kazi
hivyo imani yake ni wakandarasi kutumia vyema fursa hiyo.


Kwa upande
wake Mhandisi Emmanuel Mapigano ambaye ni mmoja wa wakandarasi waliohudhuria
semina hiyo kutoka kampuni ya MP Investment Ltd, alitoa rai kwa benki ya CRDB,
Tanroad pamoja na kampuni ya Mantrac kuendeleza ushirikiano huo ili kuwawezesha
wakandarasi kukua na kulijenga taifa kwa umoja.

Wakandarasi waliohudhuria semina hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Mwanza, Wambura Calystus.
Mkurugenzi wa CRDB, wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuke (kushoto), akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Mwanza, Wambura Calystus.
Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa kutoka kampuni ya uuzaji na ukodishaji mitambo ya Matrac, Eutachius Katiti akieleza huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
Kaimu Meneja wa Tanroad mkoani Mwanza, Mhandisi Pius Mwami akizungumza kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi CRD mkoani Mwanza, akizungumza kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya MP Investment Ltd, Mapigano John akichangia mada kwenye semina hiyo.
BMG Habari, Pamoja Daima!

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA DHAMANA YA KAZI NA MIKOPO WAKANDARASI
BENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA DHAMANA YA KAZI NA MIKOPO WAKANDARASI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDJh68FoCo8KNGD3TSF8ByyZEAoi1btA7lb0IZqIgw5sPJyU7uRDB0oMaDNFG-iTR1P2o0qBe9WEbBV8PFLXoZs6AL5F9Ezh0Xokl8Z3SHfnYI8eSr26Bs5oqxtem9xOK3Vx8OADYpFWw/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDJh68FoCo8KNGD3TSF8ByyZEAoi1btA7lb0IZqIgw5sPJyU7uRDB0oMaDNFG-iTR1P2o0qBe9WEbBV8PFLXoZs6AL5F9Ezh0Xokl8Z3SHfnYI8eSr26Bs5oqxtem9xOK3Vx8OADYpFWw/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/benki-ya-crdb-yawahakikishia-dhamana-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/benki-ya-crdb-yawahakikishia-dhamana-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy