WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM WAAPISHWA LEO, RC MAKONDA AWATAKA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es S alaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon...






 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar leo Julai 4, 2016. (PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG).
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

 Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.

Makonda alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya wanazozisimamia.

Alieleza kuwa kwa kuwa wao ndio wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.

“Ningependa wakuu wangu wa Wilaya mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu kwa kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto zilizopo katika Wilaya zao.

Aidha, Makonda amewasisitiza kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia sigara.

Wakuu wa Wilaya wapya wamepewa wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira ya kazi katika maeneo yao.

 Sehemu ya Wakuu wa Ulinzi na Usalama wa Jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye hafla hiyo.

 Sehemu ya Wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla ya  kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.

 Wakuu wapya wa Wilaya wa Jiji la Dar es salaam, toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole hakuweza kuhudhulia hafla hiyo kutokana na kupatwa na dharula. hivyo ataapishwa pindi atakapomaliza dharula yake.
 Mapitio kigo katika hati ya Kiapo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM WAAPISHWA LEO, RC MAKONDA AWATAKA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA
WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM WAAPISHWA LEO, RC MAKONDA AWATAKA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3Y222JRfd0mZx54fNX_XBGgrI7SEFRxwypexEgqeK7YUt0TxksGgVxVbwfegZPpv_XfI59tWxaQNaGf6_YOsn-rbWxIlnNTppWWNkSvQD-GckDQ0l3zA5uN8pgSIcTe7jcECWzEBvD-5A/s640/MMG_3573.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3Y222JRfd0mZx54fNX_XBGgrI7SEFRxwypexEgqeK7YUt0TxksGgVxVbwfegZPpv_XfI59tWxaQNaGf6_YOsn-rbWxIlnNTppWWNkSvQD-GckDQ0l3zA5uN8pgSIcTe7jcECWzEBvD-5A/s72-c/MMG_3573.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/07/wakuu-wapya-wa-wilaya-za-jiji-la-dar-es.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/wakuu-wapya-wa-wilaya-za-jiji-la-dar-es.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy