Na Frank Shija, MAELEZO Katika kuhakikisha heshima , hadhi na maadili miongoni mwa jamii ya Watanzania Serikali ya Awamu ya Tano c...
Na Frank Shija, MAELEZO
Katika kuhakikisha heshima , hadhi na
maadili miongoni mwa jamii ya Watanzania Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
uongozi mahiri wa Rais John Pombe Magufuli imewakumbusha wananchi kuheshimu na kuzingatia matumizi sahihi ya
Vielelezo vya Taifa.
Haya yamebainishwa na Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali Cassian Chibogoyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
katika Kipindi chake cha ‘Tujikumbushe’’ Sehemu ya Pili kilichofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Chibogoyo amesema amesema kuwa wakati
sasa umefika kwa jamii kuendeleza utamaduni uliokuwapo wa kuheshimu na kufuata
desturi zilizowekwa katika kuendeleza umoja, amani na mshikamano.
‘Natoa wito kwa watanzania wote, katika
kufanya maboresho ya kurejesha hadhi ya taifa tunapaswa kuheshimu sana
Vielelezo vya Taifa letu, hapa na maanisha tuheshimu wimbo wa taifa na Nembo ya
Taifa.’
Amesema kuwa katika kuhakikisha
vielelezo hivyo vinaheshimiwa Ofisi yake imejipanga kufuatilia kwa karibu wale
wote watakao kiuka matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa ikiwemo Nembo,
Bendera na Wimbo wa Taifa.
Aliongeza kuwa kuanzia sasa matumizi ya
Bendera ya Taifa yatakwenda sambamba na matumizi ya Bendera ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki hivyo amezitaka Ofisi zote za Serikali pamoja na Taasisi zake
waanze utaratibu wa kupandisha pia bendera hiyo kwani Tanzania tunaamini katika
ushirikiano huo.
Katika hatua nyingine uongozi wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu (TUGHE) Tawi la Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali wamekanusha tuhuma zilizoandikwa na moja ya gazeti hapa nchini(Jina
limehifadhiwa) zikimtuhumu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa na kusema kuwa
tuhuma zilizoandikwa katika Gazeti hilo siyo zakweli na ata wao kama wafanyakazi
wameshangazwa
Katibu wa TUGHE Tawi la Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali amesema kuwa ni vyema waandishi wakafanya kazi zao kwa weledi
kuliko kuandika taarifa zizizosahihi kwani kufanya hivyo kuta waingiza
matatizoni.
Nilitegemea kabla mwandishi hajachapisha
habari ile angetafuta ukweli kutoka upande wa pili ikiwemo kuhusishwa kwa
uongozi wa Chama cha Wafanyakazi kwani ndiyo wenye mamlaka yakutoa taarifa
katika ngazi husika kwa tupo kwa ajili ya kuwawakilisha na kuwatetea
wafanyakazi.
Kipindi cha Tujikumbushe kimekuwa
kikionyeshwa na TBC1 ambapo lengo lake kuu ni kutoa elimu kwa jamiii juu ya
matumizi sahihi na umuhimu wa kutunza nyaraka na tunu za Taifa, ambapo Sehemu
ya Kwanza ya kipindi hicho kilihusu Nyaraka za Serikali. Kipindi kinachofuata
kitahusu Historia ya kuwepo kwa Katiba na Katiba inayopendekezwa.
COMMENTS