Na Selemani Semunyu, JWTZ Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Issa Nasso...
Na Selemani Semunyu, JWTZ
Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Issa Nassoro amezitaka Timu teule za
Jeshi kutobweteka na Ushindi wanaoupata katika mechi za majaribio wanazocheza.
Kauli hiyo imekuja Mwisho mwa wiki wakati Timu ya Mpira wa Pete (Netball) Wanawake ya jeshi
la Wananchi wa Tanzania kudhihirisha ubabe wake baada ya kuifunga Timu ya Mpira
wa pete ya Wananume ya kikosi cha Valentia Zanzibar -KVZ kwa Magoli 36 kwa 24 katika
mchezo uliofanyika Mwishoni mwa wiki Visiwani Zanzibar
Mchezo huo uliofanyika Katika katika uwanja wa Polisi
Bwawani Ulikuwa kivutio kikubwa kutokana na kuhusisha jinsi mbili tofauti kwa maana ya Wanaume na Wanawawake lakini pia
ukiwa na wachezaji mahiri kutoka katika Timu zote mbili ambao wamekuwa na
majina makubwa katika mchezo huo.
Meja Jenerali Nassoro aliyekuwa katika Ziara ya kutembelea
kambi ya Timu teule za jeshi za mpira wa Miguu,Pete,Kikapu na Mpira wa Mikono zilizoweka kambi katika
Visiwa vya Unguja Mjini Zanzibar alisema ameridhishwa na kambi licha ya
Jitihada zaidi kuongezwa ili kujihakikishia ushindi.
Alisema anamatumaini Makubwa
historia ya kuweka kambi Zanzibar kutazibeba Timu za Jeshi kwani Timu
mbalimbali zilizowahi kuweka kambi Zanzibar zilipata Mafanikio hivyo Jeshi na Taifa
tunategemea hilo kama eneo zuri kwa kambi ili kujiandaa vizuri.
“Niliamua kwa Makusudi kupendekeza kambi kuwa Zanzibar
nimekuwa Mchezaji na Mwanamichezo muda mrefu najua faida za kuweka kambi Zanzibar
ukilinganisha na maeneo mengine kama Dar es Salaam” Alisema Meja Jenerali Nassoro
Katika michezo ya majaribio za
Timu hizo Teule za jeshi Katika Mchezo
wa mpira wa Kikapu Timu ya Jeshi wameifunga Timu ya Mbuyuni kwa Vikapu 104 kwa
58 na kuifanya Timu hiyo kuendeleza ubabe ikiwa ni mchezo baada ya michezo yake
ya Awali kuzifunga Timu mabingwa wa Mchezo huo kwa Zanzibar.
Timu hizo zilizochezea kichapo katika Mpira wa Kikapu JWTZ iliifunga Stone Town kwa Vikapu 69 kwa 48
wakati mchezo uliochezwa kabla JWTZ waliifunga polisi kwa Vikapu 68 kwa 49
michezo iliyochezwa katika Viwanja Vya Maisara.
Katika hatua Nyingine Timu ya Soka ya JWTZ inakumbukumbu ya
kuifunga Mafunzo kwa mabao Mawili kwa moja ikiwa ni mchezo wa marudiano huku
mchezo wa Kwanza Timu ya Jeshi ikiwa imeibuka kwa Ushindi wa mabao Mawili kwa
Moja, Katika mchezo Mwingine JWTZ wameifunga jeshi la Kujenga Uchumi JKU kwa
Magoli Mawili kwa Moja.
Katika Mpira wa Mikono JWTZ wameifunga Vijana Combine kwa Magoli 37
kwa 16 wakati katika Mchezo mwingine JWTZ waliifunga Zanzibar Warriors kwa Magoli
36 kwa 16.
COMMENTS