MAONESHO YA BEAUTY SALON KUANZA FEBRUARI 7 MSASANI DAR ES SALAAM

Mratibu wa maonesho ya Beauty Salons and Beast, Jan van Esch akiongea na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo yanayoanza Msasani en...
Mratibu wa maonesho ya Beauty Salons and Beast, Jan van Esch akiongea na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo yanayoanza Msasani eneo la Eddo chips mkabala na kituo cha Polisi cha Oysterbay Dar es Salaam. Kutoka (kushoto) ni Mratibu mwenza, Rehema Chachage, na wasanii Cloud Chatanda, Gadi Ramadhani na Amani Abeid.

******************************BEAUTY SALONS AND THE BEAST
(SALUNI ZA UREMBO NA URIMBO)
Mwisho wa siku…sanaa ya umma…inahusu sanaa na umma. Na hilo litaendelea kuwa hivyo pale ambapo huo umma siyo tu kikundi kidogo cha watu wanaojua na kufuatilia sanaa, bali ni mchanganyiko wa taifa lenye matabaka, fursa tofauti, viwango mbalimbali vya kuwa na muda wa kutosha; hivyo basi, sanaa ya umma hakika itakuwa ni ya umma pale tu inapohusu vilivyo vya umma.’
Mwaka 2008 nilishuhudia uzinduzi wa kile ambacho sasa kimekuwa tamasha maarufu sana la sanaa duniani lijulikanalo kama Infecting The City, yaani ‘Kuliambukiza Jiji’. Hili ni tamasha linaloshirikisha aina nyingi za sanaa na maonyesho katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini na hivyo kutoa nafasi na fursa kwa mtu yeyote kuzifikia na kuona kazi mbalimbali za sanaa. Kipindi hicho nilikuwa ndiyo kwanza naanza mwaka wangu wa tatu wa masomo ya Shahada ya kwanza ya Sanaa, hivyo, hata sikujua mwelekeo wangu kitaaluma na kisanii utakuwaje. Lakini nakumbuka jinsi gani wazo la walioanzisha tamasha hilo lilivyonigusa na kunifanya nitamani siku moja na sisi tuazime hata sehemu ndogo tu ya wazo hilo ili kuwe na tamasha kama hilo katika jiji letu la Dar es Salaam, Tanzania. Pia nilitamani niwe mmoja wa waandaaji wa tamasha la aina hiyo jijini Dar es Salaam kwa kadri vionjo, uwezo na muktadha wetu utakavyoruhusu. Hatimaye mwaka huu, ikiwa ni mwaka wa nane toka niupate ule uzoefu ulionigusa kwa mara ya kwanza, nimefanikiwa kuifikia azma hiyo kupitia maonyesho ya Apexart Franchise tuyaitayo “Beauty Salons and the Beast”, yaani, 'Saluni za Urembo na Urimbo.’

Tamasha la Saluni za Urembo na Urimbo ni zao la wasanii wawili – mimi mwenyewe, Rehema Chachage, na Jan van Esch – ambao pia tupo kwenye menejimenti ya taasisi ijulikanayo kama Nafasi Art Space, kituo pekee cha sanaa ya kisasa jijini Dar es Salaam. Wazo la kuwa na tamasha hili liliibuka kufuatia hali tuionayo Tanzania, yaani: kuhudhuria maonyesho ya sanaa kiukweli siyo utamaduni wa Watanzania walio wengi. Hivyo, ukilinganisha na raia wa kigeni, hakuna Watanzania wa kutosha wanaohudhuria maonyesho ya utamaduni pamoja na matukio mengine ya kiutamaduni katika vilinge vya tamaduni jijini. Sisi kama waandaaji wa takribani asilimia 50 ya maonyesho hayo, mara kwa mara tunajikuta tukijiuliza umma wa Watanzania uko wapi na ni kwa namna gani tunaweza kufanya iwezekane kwa umma huo kupata fursa ya kuona sanaa na kuwafikia wasanii.

Baada ya kubunga bongo na kutafakari sana, tukahitimisha kuwa labda njia pekee ya kuweza kuwafikia watu wengi zaidi ni kwa kuazima mbinu ya ‘Kuambukiza Jiji’ na kujaribu kufanya maonyesho yanayoibuka ‘papo kwa hapo’ katika maeneo ya umma ili kuvutia mkusanyiko mkubwa wa Watanzania. Tunasema, ‘Kama hawataifuata sanaa, basi tuiachie sanaa iwafuate wao;’ na tupo kwenye mkakati wa kuwafuata (umma wa) watazamaji wa sanaa popote pale walipo. Katika jaribio hili la kwanza la maonyesho ya ‘papo kwa hapo’, tumeamua kutumia saluni kama maeneo ya maonyesho baada ya kuona makala ya Beauty Salons and the Beast (yaani Saluni za urembo na Urimbo) iliyoandikwa na Erick Mchome. Makala hiyo inaonyesha ni kwa kiwango gani saluni zimekuwa ni biashara zinazokuja juu kwa kasi jijini Dar es Salaam ambapo tunaona kundi kubwa la watu wa matabaka ya juu, kati na chini ya kiuchumi/kimaisha nchini Tanzania yakitumia muda wao wa ziada humo, hasa mwisho wa wiki, yaani, wikiendi. Hawa ndiyo aina ya watazamaji ambao maonyesho yetu yanalenga kuwafikia.
Katika jaribio hili la kwanza la maonyesho ya ‘papo kwa hapo’, tumeona ni vyema tujaribu kwanza kutumia saluni zilizoko katika maeneo ya karibu na tulipo, hivyo tumechagua eneo la Msasani ambalo kiutawala ni kata katika Wilaya ya Kinondoni. Msasani pia ipo kati ya Peninsula (yaani maeneo ya Masaki/Oysterbay), ampapo wanaishi wageni wengi pamoja na Watanzania wengi wa daraja/tabaka la kati na la juu kiuchumi/kimaisha, na Kijiji cha Msasani ambacho zamani kilikuwa ni kijiji cha wavuvi na mpaka sasa kina mkusanyiko mkubwa wa watanzania wa tabaka la chini kiuchumi. Hali kadhalika ni rahisi kwa watu wengine kutoka maeneo mengine ya Wilaya ya Kinondoni (wengi wao wakiwa ni mchanganyiko wa tabaka la chini na la kati kimaisha/kiuchumi) kupafikia Msasani maana biashara nyingi zinazowahudumia ziko hapo. Hivyo mazingira hayo yanatupa fursa ya kuwafikia Watanzania wengi na wa aina nyingi ambao kwa kawaida hatuwaoni kwenye maonyesho ya wazi ya usiku tuyafanyao katika kituo chetu cha Nafasi Art Space.
Kama walivyo wasanii wengi wanaongezeka leo, wasanii waliochaguliwa kwa ajili ya maonyesho ya Saluni za Urembo na Urimbo wanapendelea sanaa ya umma na kuhoji nafasi zao katika jamii kwa kutumia sanaa kuwasiliana na jamii husika kuhusu masuala muhimu ya kijamii. Wanatumia maonyesho haya kama mbinu ya kuitoa sanaa kwenye kuta nne za kituo cha sanaa walichokizoea na kuzipeleka nje kwa watu ambao siyo kawaida yao kuja kwenye vituo vya sanaa. Kwa kuwafikia watu hao, wasanii hawa pia wanapata fursa ya kusikiliza maoni mbadala kuhusu ujumbe wao wa kisanii na hivyo kuwawezesha kukuza maono na usikivu wa vionjo na tafsiri za Kitanzania kuhusu sanaa ya kisasa. Kupitia kitendo hiki, wasanii wanataka kuwapa changamoto watazamaji na wao wazingatie na watazame kwa undani zaidi mazingira waliyopo – yaani, muktadha ambao sanaa yao inapokelewa nao na mitazamo inayoibuka humo ni masuala muhimu katika maonyesho haya. Kwa namna fulani, wasanii hawa wanachukua nafasi ya watetezi (kupitia sanaa) wa mitazamo mbadala inayohoji tafsiri, imani na misimamo ya jamii.
Kuna njia nyingi za kutafsiri mitazamo na maana ya mchango wa kila msanii. Sisi kama wasimamizi wa maonyesho haya ya Saluni za Urembo na Urimbo, tumetoa fursa kwa mtazamo na tafsiri yoyote ile ambayo wasanii wataiongezea kwenye wazo letu la kuwa na maonyesho haya. Japokuwa kila mada ya msanii katika nafasi yake imejikita kwenye taaluma au mfumo fulani wa sanaa, mnyanganyiko wa uzoefu wa  ndani na wa nje wa wasanii wote, kwa pamoja, ni mpana na unaakisi uzoefu wa nchi yetu na siasa zake katika mapana yake.
Maonyesho yaliyojumuishwa katika Saluni za Urembo na Urimbo ni yale ambayo yanagusa fikra zetu na kugusia kipindi hiki na mazingira yetu ya sasa nchini. Mengi yanagusia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 na kurejea miaka 5+ ya Uhuru na miaka 20+ ya mfumo wa demokrasia ya kiliberali pamoja na mikanganyiko yake, mmojawapo ukiwa ni namna ya kuzuia rushwa/ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Kwa kuzingatia upigaji kura, wasanii kwa pamoja walikubaliana tuanze na mfumo wa maswali ya kuchagua kama mbinu ya kwanza na mada mtambuka – kama namna ya kutathmini ambapo watu wanaulizwa wachagua jibu au majibu kutoka kwenye orodha ya majibu, mtu hugudua kuwa mara nyingi jibu linakuwa ni majibu yote, yaani kuna mengi ya kuchagua.
Jan van Esch na Aika Kirei, kwa mfano, wanatumia ‘mbinu ya kutathmini kwa kutumia maswali ya kuchagua’ kuuliza maswali kuhusu namna ambavyo wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati wanavyopata au kukosa fursa. Na, kama ilivyokuwa kwa baba yake aliyekuwa Profesa wa Sosholojia na Mchambuzi wa masuala ya Kijamii  na ambaye anasemekana kuwa mtu wa kwanza kuyachezesha kikejeli maneno ya kaulimbiu ya chama tawala ya uchaguzi wa mwaka 2005, Rehema Chachage naye anayachezea kisanii maneno hayo ya ARI, NGUVU, KASI ambayo kiuhalisia yamekuwa kinyume chake na kuwa A, -NGU, -KA (ANGUKA) kutokana na chama hicho kushindwa kutekeleza mambo mengi waliyoahidi. Vivyo hivyo, japo kwa mbinu tofauti, Gadi Ramadhani anatumia mwendelezo wa maonyesho yake ya Blindfolded (Kufungwa Macho) kuonyesha, kwa mtazamo wa kisanii, ni jinsi gani leo sisi kama jamii tumefungwa kitambaa machoni hivyo ni kama vile tunatembea bila kujua/kuona jinsi ambavyo mfumo tawala (wanasiasa, vyombo vya habari n.k.) unatuhadaa.
Kwenye suala la maamuzi na kuchagua, Delphine Buysse  anatumia madoli 50 yanayoning’inia kichwa chini miguu juu na ambayo yamepakwa rangi ya kijivu kwa asilimia 50, kuonyesha na kuchambua mtanziko wa maisha na ugumu utokanao na kuamua/kuchagua. Eneida Sanches naye analitazama suala hilo hilo ila kwa namna tofauti. Kwa kutumia michoro ya wanaume ambao hawapo (tena) katika maisha yake, sanaa yake inaonyesha mikanganyiko na tafakuri kuhusu wanaume hao na uchaguzi/uamuzi wao wa kumwacha… swali lake kuu likiwa ni; wako wapi na nini kiliwafanya waondoke/wamwache?
Cloud Chatanda anakuja na mtazamo chanya zaidi kwenye mada hii kwa kutumia mchanganyiko tete wa uchoraji na uchongaji kuonyesha jinsi viumbe vya zamani visivyojulikana ambavyo kwa muda mrefu vimegana kwenye Mlima Kilimanjaro vinaamka na kukuta Tanzania iliyo katika hali tata na kuamua kupambana na matatizo ili kulirudisha Taifa kwenye hali yake ya asili. Hali kadhalika Amani Abeid naye anakuja na mtazamo chanya kwa kuonyesha shujaa anaejitokeza (kutoka Tanzania) kuikoa dunia kutoka kwenye majanga baada ya mashujaa maarufu na wapendwao wa nchi za magharibu kushindwa kufanya hivyo.
Onyesho la Vita Maluli, ambalo limejikita zaidi kwenye kejeli, linatumia ‘kango moko’, yaani kipande kimoja cha kanga chenye vijimaneno au vijembe, ambapo tunaona kanga ikiwa imepata uhuru zaidi hivi karibuni baada ya kuacha utamaduni wa kuwa tu vazi la kuvaliwa nyumbani kwa matumizi ya ndani na kuwa pia vazi linaloonekana mitaani, likiwa limevaliwa na wanawake mchana kweupe.
Kila msanii anajaribu, kwa namna yake ya pekee, kupaza sauti yake kuelezea yale yanayomgusa. Kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Afrika, Tanner Methvin anavyosema, “propaganda ni kusema hatuna mamlaka ya kujieleza kwa Uhuru. Eti sauti zetu zinahitaji ruhusa kutoka kwa mtu au kitu fulani chenye mamlaka hayo. Kuwa walimu wetu, wakuu wa taasis za elimu, mabosi wetu, na maofisa wa Serikali ndiyo wanaturuhusu kucheza muziki, kuimba, kuchora, kupiga picha, kuandika, au hata kuongea tu. Wanatuambia lini tumechaguliwa au tumeteuliwa na hapo ndipo tu tunaposimama…Hili kwa hakika ni hekaya lakini ambayo tunashiriki kuitunga na kuikuza kila mara tunapojibana wenyewe na kuzikimbia fursa za kuelezea visa vyetu wenyewe.”

Rehema Chachage (Msimamizi wa maonyesho, Beauty Salons and The BeastSaluni za Urembo na Urimbo)
*****************PRESS RELEASE: LAUNCH OF BEAUTY SALONS AND THE BEAST EXHIBITION AND INTERVENTIONS

FOR IMMEDIATE RELEASE.

The launch of ‘Beauty Salons and the Beast’; an art exhibition featuring interventions in beauty salons and barbershops of Msasani area, Dar es Salaam. The exhibition will feature artworks and interventions from the following artists;

Amani Abeid (Tanzania)
Delphine Buysse (Tanzania/Belgium)
Rehema Chachage (Tanzania)
Cloud Chatanda (Tanzania)
Eneida Sanches (Brazil)
Jan Van Esch (Tanzania/Netherlands)
Aika Kirei (Tanzania)
Vita Malulu (Tanzania)
Gadi Ramadhani (Tanzania)

On view:
February 7 - March 7, 2015
In beauty salons and barbershops of the Msasani area (Makangira street near Edo Chips), Dar es Salaam, Tanzania

Synopsis:
Beauty Salons and the Beast will introduce the Tanzanian public to new and experimental art and attempt to increase public interest and dialogue in the happenings and role of the visual arts in Tanzania. The project carries the theme of ‘multiple-choice’ and will feature artworks and interventions from local Tanzanian and international artists.

Beauty Salons and the Beast is interested in the public sphere and in questioning the role of artists in society by using artistic media and creative expression to engage with communities to communicate, explore and articulate issues of local significance. It employs the ‘if they don't follow the art, we will bring the art to them’ module by ‘infecting the city’ with activities like public performances, interventions and public discussion as a way of ‘bringing art’ to the community, and as a dialogue starter.

The launch for the project will be on 7th February 2015 at 14.00hrs and will feature exhibited works of art in a total of 4 small and large beauty salons and barbershops located in Makangira Street (Also known as Msasani street near Edo Chips) in Dar es Salaam. The launch will feature entertainment, and speeches from the organizing team, the artists as well as the sponsors for the project; apexart an organization based in New York, USA.
Beauty Salons and the Beast is organized by Rehema Chachage and Jan van Esch
 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAONESHO YA BEAUTY SALON KUANZA FEBRUARI 7 MSASANI DAR ES SALAAM
MAONESHO YA BEAUTY SALON KUANZA FEBRUARI 7 MSASANI DAR ES SALAAM
http://2.bp.blogspot.com/-Vi6ZtN04GWU/VNSz37WDzjI/AAAAAAAAm20/bdFVu4N1EdU/s1600/MOJA.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-Vi6ZtN04GWU/VNSz37WDzjI/AAAAAAAAm20/bdFVu4N1EdU/s72-c/MOJA.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2015/02/maonesho-ya-beauty-salon-kuanza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/02/maonesho-ya-beauty-salon-kuanza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy