Mwanasheria Mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, a...
|
Mwanasheria Mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Othman
Masoud Othman, amefutwa kazi na mteule wake, rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa
baraza la mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein.
Tayari Dkt. Shein amemteua aliyekuwa naibu mwanasheria mkuu,
Said Hassan Said, kuchukua nafasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali,iliyopatikana Oktoba 7,
2014 kwa vyombo vya habari Masoud amefutwa kazi kwa mujibu wa vifungu namba 53
na 54 (1) na 55 (3) vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, na kifungu namba 12
(3) sheria ya utumishi wa umma ya Zanzibar ya mwaka 2011.
Itakumbukwa ya kwamba, Masoud, alijiondoa kwenye kamati ya uandishi
ya bunge maalum la Katiba, bila ya kutoa sababu zozote huku akiwa mshauri
mkluu wa sharia wa serikali hiyo na alionekana siku ya pili ya upigaji kura
kuamua hatma ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa na
bunge hilo.
Jambo lililowashtua wengi, katika kura yake ambayo ilikuwa
ya wazi, alipiga kura ya hapana akikataa vifungu kadhaa vya katiba hiyo, hali
iliyoamsha hamasa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa b unge hilo kutoka Zanzibar,
na kupiga makelele ya kutaka aondolewe kwenye nafasi hiyo.
Hali hiyo iliwalazimu maafisa wa usalama wa bunge hilo,
kumpatia ulinzi maal;um wakati akiondoka bungeni hapo ili kumuepiusha na kipigo
kiutoka kwa wajumbe wa Bunge hilo.
|
|
Mwanasheria Mkuu mpya wa serikali ya mapinduzi, Zanzibar, Said Hassan Said. |
|
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein |
|
Spika
wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, (kushoto),
akiteta jambno na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi
Zanzibar, Othman Masoud Othman, mwanzoni mwa vikao vya bunge maalum la
katiba mjini Dodoma. |
|
Askari
wa bunge wakimsindikiza mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi
Zanzibar, Othman Masoud Othman, (Wa pili kulia), wakatin akitolewa kwenye
ukumbi wa bunge hilo kupitia mlango wa nyuman kumuepusha na kipigo toka
kwa wajumbe kutoka Zanzibar. Kulia ni spika wa baraza la wawakilishi
Pandu Ameir Kificho, ambaye alitumia gari lake kumtorosha kutoka viwanja
vya bunge. (Imeandaliwa na K-VIS Blogs) |
COMMENTS