WAZIRI MPINA AJA NA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina,akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/2019 bungen...WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina,akiwasilisha
mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/2019 bungeni
jijini Dodoma jana. Picha na John Mapepele 

*Viwanda vya nyama vilivyokufa kufufuliwa,Narco kusukwa upya

*Kuanzisha Mamlaka ya kusimamia uvuvi,Tafico kufufuliwa

 

Na John Mapepele, DODOMA

WAZIRI
 wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema kuwa  Wizara inafanya mageuzi
makubwa kwenye sekta ya Uvuvi, kwa kuanzisha Mamlaka ya kusimamia
rasilimali za uvuvi ili kuleta suluhisho la kudumu katika kunusuru
rasilimali hizo ambazo kwa sasa zinavunwa kiholela,kutoroshwa nje ya
nchi na Serikali kukosa mapato.


Akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa
mwaka 2018/2019 bungeni jijini Dodoma jana, Mpina alisema Serikali pia
itahakikisha  inafufua  Shirika la Taifa la Uvuvi,TAFICO  na kufufua
vituo vyote vya kuzalisha vifaranga vya samaki ili wananchi wengi zaidi
waweze kupata mbegu bora ya samaki na kufuga kibiashara sambamba na
kuanzishwa kwa bandari ya Uvuvi.

Mpina alisema Wizara itafufua
viwanda  vyote vya nyama ili  mifugo yote nchini iweze kuuzwa  na 
kuchinjwa kwenye viwanda hivyo na kuliingizia taifa mapato. Alivitaja
baadhi ya viwanda vitakavyofufuliwa kuwa ni  kiwanda cha nyama cha
Shinyanga, Mbeya, Utegi na Mwanza.

Pia alisema wizara imejipanga
 kulisuka upya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ili liweze kuzalisha
kibiashara zaidi tofauti na hali ilivyo sasa ambapo alisema  Wizara
imeandaa mkakati  mpya wa kuvunja mikataba yote isiyo na tija na
kuwaondoa wawekezaji ambao wameshindwa kukidhi matakwa ya uwekezaji.

Pia
 kuweka ulinzi  ulinzi imara na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato
ambayo itawezesha kuongezeka kwa mapato zaidi ya mara 10 ya ilivyo sasa
ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na
Mamlaka za Serikali za Mitaa zitaendelea kufanya operesheni hadi
kuutokomeza uvuvi na biashara haramu.

Akiwasilisha mpango na
makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/2019 bungeni
jijini Dodoma jana Waziri Mpina alisema Serikali pia itaendelea uendelea
 kuzielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao ya
kusimamia, kutunza na kuendeleza rasilimali za uvuvi katika maeneo yao
na kuweka miundombinu kwa ajili ya shughuli za uvuvi.

Pia
kuandaa utaratibu wa kuwezesha Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Idara ya
Uvuvi) kusimamia Mialo na Masoko ya Kimataifa ya Samaki badala ya
Halmashauri kama ilivyo hivi sasa kuendelea kuwachukulia hatua Watendaji
 wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaojishughulisha na uvuvi na biashara
haramu kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma

Pia
 kushauri Mamlaka husika kuwachukulia hatua viongozi wa kisiasa na
watendaji wa Serikali wanaoshiriki na kufadhili uvuvi haramu na
kuishauri TRA ifanye makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara wa mazao ya
uvuvi waliokwepa kulipa mapato ya Serikali mwaka 2016/2017 ambapo
inakadiriwa kuwa mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 581.5
hayakufanyiwa makadirio na TRA na hivyo kuikosesha mapato Serikali.

Pia
 katika mwaka 2018/2019, Wizara kwa kushirikiana na wadau itaendelea
kusimamia na kuimarisha usimamizi na ulinzi wa rasilimali za uvuvi kwa
kufanya doria za kawaida zenye siku kazi 6,000. Aidha, itawezesha MATT
kutekeleza kazi zake kwa kufanya operesheni 12 katika maji bahari na
kupanua majukumu ya MATT hadi maji baridi. Vilevile, Wizara itaendelea
kutoa elimu na mafunzo kwa wavuvi na wadau wengine kuhusu madhara ya
uvuvi haramu na faida za uvuvi endelevu.
 
Alisema katika mwaka
2017/2018, Wizara kupitia Fungu 64 ilipangiwa kukusanya kiasi cha
shilingi19,700,628,051.00 ambapo hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2018
kiasi cha shilingi 21,280,222,364.48 kimekusanywa na Wizara ikiwa ni
sawa na 108.02%  ikilinganishwa na shilingi 16,019,668,687.00
zilizokusanywa kuanzia mwezi Julai 2016 hadi tarehe 30 Aprili 2017.
Katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Fungu 64 inatarajia kukusanya
jumla ya shilingi 21,534,305,600.00.

Pia katika mwaka 2018/2019,
 Wizara kupitia Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu itakamilisha
Sera ya Uvuvi wa Bahari Kuu. Pia, itaendelea kutekeleza Mkakati wa
Kuboresha Sekta ya Uvuvi na Programu ya KuendelezaSekta ya Kilimo Awamu
ya Pili (ASDP II).

Vilevile, wizara itafanya mapitio ya Mpango
Kabambe wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Fisheries Master Plan) wa mwaka 2015
 na kuendelea na taratibu za kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
ambapo shilingi bilioni 45 zinahitajika kwa ajili ya kuanzisha upya
Shirika hili. Kuwepo kwa shirika hili kutawezesha nchi yetu kuwa na meli
 za kitaifa (National Fleet) kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu ili
kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la Taifa.

Pia,
Wizara itakamilisha mapitio ya Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003;
Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na. 29 ya mwaka 1994 ili
kupanua maeneo ya hifadhi kwenye maji baridi na Sheria ya Mamlaka ya
Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu Na. 1 ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya
mwaka 2007 na kuandaa kanuni mpya za kutekeleza Sheria mpya ya Uvuvi.

Alisema
 katika kipindi cha Julai, 2017 hadi Aprili, 2018 uzalishaji wa maziwa
umefikia lita bilioni 2.4 ukilinganishwa na lita bilioni 2.1
zilizozalishwa katika kipindi cha Julai, 2016 hadi Aprili, 2017. Aidha,
katika kipindi hiki usindikaji wa maziwa umeongezeka na kufikia lita
milioni 56.2 ikilinganishwa na maziwa lita milioni 40.1
zilizoshindikwakatika kipindi cha Julai, 2016 hadi Aprili, 2018.

Pia,
 katika kipindi hiki, jumla ya mitamba 590 ilizalishwa kutoka katika
mashamba ya Serikali na ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Vilevile,
 Sekta Binafsi ilizalisha na kuuza kwa wafugaji wadogo nchini jumla ya
mitamba 13,145.

Aidha katika kipindi cha Julai, 2017 hadi
Aprili, 2018, uzalishaji wa zao la nyama umeongezeka kufikia tani
679,992 ikilinganishwa tani 558,164 zilizozalishwa katika kipindi Julai,
 2017 hadi Aprili, 2018. Aidha, katika kipindi cha Julai, 2017 hadi
Aprili, 2018, jumla ya tani 2,608.93 za nyama ziliuzwa nje ya nchi na
jumla ya tani 1,224.55 za nyama ziliingizwa nchini. Pia, uzalishaji wa
mayai uliongezeka nchini kutoka mayai bilioni 2.76 mwaka 2016/2017 hadi
bilioni 3.16 mwaka 2017/2018.

Pia ulaji wa nyama kwa mwaka
2017/2018 ni wastani wa kilo 15, lita 47 za maziwa na mayai 106 kwa mtu
kwa mwaka ikilinganishwa na viwango vya Shirika la Chakula na Kilimo la
Umoja wa Mataifa (FAO, 2011) ambavyo ni kilo 50 za nyama, lita 200 za
maziwa na mayai 300 kwa mtu kwa mwaka.

Alisema katika mwaka
2017/2018, Wizara kupitia Fungu 99 (Maendeleo ya Mifugo) ilipangiwa
kukusanya shilingi16,404,739,500.00. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2018
 kiasi cha shilingi 13,677,333,381.24 kimekusanywa, sawa na83.4%,
ikilinganishwa na shilingi 10,952,827,50 zilizokusanywa mwaka 2016/2017
kuanzia mwezi Julai, 2016 hadi tarehe 30 Aprili, 2017. Katika mwaka
2018/2019, Wizara kupitia Fungu 99 inatarajia kukusanya jumla ya
shilingi18,467,945,100.00.

Hivyo katika mwaka 2018/2019, Wizara
itaimarisha mashamba matano (5) ya kuzalisha mitamba ya Sao Hill,
Kitulo, Ngerengere, Nangaramo na Mabuki kwa kununua mitamba aina ya
boran 1,000 na madume bora aina ya Friesian 200 na boran ili kuongeza
idadi ya ng’ombe wazazi na kuboresha malisho na miundombinu ya maji.
Aidha, Wizara itaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuongeza uzalishaji
wa mitamba na kusambaza kwa wafugaji. Pia, Wizara imeanzisha Programu ya
 uzalishaji wa mitamba 1,000,000 kwa mwaka kutokana na makundi ya
ng’ombe wa asili kwakufanya uhimilishaji katika ng’ombe milioni 3.0 kwa
ajili ya kuongeza uzalishaji maziwa ili kukidhi mahitaji.

Waziri
 Mpina alisema katika mwaka 2018/2019, Wizara itaendelea  kuimarisha
Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha NAIC Usa River, Arusha kwa kununua
vitendea kazi na kukarabati mabanda ya madume na kuendeleza malisho.

Pia,
 Wizara itajenga kituo cha NAIC Sao Hill Iringa, itanunua trekta na
vifaa vyake na kutoa mafunzo kwa wahimilishaji 200 kutoka mikoa 10 ya
Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Kigoma,
Katavi na Geita. Aidha, itaimarisha vituo sita (6) vya Kanda vya
uhimilishaji vya Dodoma, Kibaha, Lindi, Mbeya, Mpanda na Mwanza kwa
kufanya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha kimiminika baridi cha
Naitrojeni, pamoja na vituo vidogo vya uhimilishaji vya Tanga na Tabora.


Hata hivyo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Heifer
International kupitia mradi wa EADD II inatarajia kupanuawigo wa mradi
huu ili kufikia maeneo mengi. Pia, itaendelea kushirikiana na Serikali,
wafugaji na wadau wengine katika kuanzisha vituo vya kisasa vya
kukusanya maziwa ili wafugaji wengi zaidi waweze kuvifikia kwa karibu
zaidi. Pia, mradi utaendelea na programu ya unywaji wa maziwa shuleni
kwa kuwafikia wanafunzi wengi zaidi katika maeneo ya mradi.

Pia
katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mifugo
Tanzania (TALIRI) itaendelea kutekelezaMradi wa Kuboresha Mbari za Kuku
wa Asili Afrika kwa ufadhili Taasisi ya Bill & Mellinda Gates
Foundation ambao unatekelezwa kwa pamoja na nchi tatu za Ethiopia,
Tanzania na Nigeria kwa miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2015 hadi 2019.
Lengo kuu la mradi ni kuongeza tija katika uzalishaji wa kuku wa asili
kwa ushirikishwaji wa sekta ya umma na sekta binafsi, hivyo kuongeza
upatikanaji wa kuku bora na kuongeza tija; kipato na uhakika wa lishe.

Kuhusu
 ‘Operesheni Nzagamba’ Waziri Mpina alisema hadi kufikia t Mei, 8 mwaka
huu jumla ya shilingi 1,992,804,200 zimekusanywa kama ushuru, tozo na
faini mbalimbali katika operesheni hiyo.

Aidha katika mwaka
2018/2019, Wizara itaendelea kuimarisha mikakati ya kulinda rasilimali
za mifugo na mazao yake kwa kuboresha vituo 36 vya ukaguzi vya mipakani.
 Pia, Wizara itashirikiana na TRA, TFDA na taasisi nyingine zaSerikali
kudhibiti uingizaji na utoaji holela wa mifugo na mazao yake kwa lengo
la kuhakikisha kuwa biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya
nchi inafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni.

“Wizara yangu
imeandaa pendekezo la kuibadilisha NARCO kutoka Kampuni kuwa Shirika la
Umma (Public Corporation) ili kuondoa utata uliopo na kupanua wigo wa
kutekeleza majukumu yake. Faida za kubadilisha NARCO kuwa Shirika la
Umma ni pamoja na kuondoa mkanganyiko wa kisheria uliokuwepo katika
muundo na uendeshaji wa Kampuni na kuwa na shirika lenye uwezo, mamlaka
na uwanda mpana zaidi wa kuleta tija kwenye sekta ya mifugo hapa nchini
na kuwa na dira, malengo na majukumu yanayotekelezeka na
kupimika”alisema.

Hivyo NARCO kwa kushirikiana na Msajili wa
Hazina na Mwanasheria Mkuu wa Serikali itahakikisha Vitalu 23 vya
wawekezaji ambao wameshindwa kuwekeza zaidi ya 50%  mikataba yao
itavunjwa kabla ya Juni 2018; Pia Vitalu 24 vya wawekezaji ambao
wameshindwa kulipa pango la ukodishaji ranchi mikataba yao itavunjwa
kabla ya Juni 2018; na wawekezaji waliokidhi masharti na matakwa ambao
wamewekeza zaidi ya 50% na kulipa ada za pango mikataba yao itahuishwa
mwezi Juni, 2018.

Kuhusu Mkataba kati ya Serikali na Viwanda vya
 Sukari vya Kagera na Mtibwa, Waziri Mpina alisema timu iliyoundwa
ilibaini mambo muhimu ambayo ni pamoja na Makampuni haya kumilikishwa
ardhi yenye ukubwa wa hekta 75,000 (sawa na ekari 187,500) bure bila
kulipia fidia ya ardhi kwa NARCO.

Pia, hakuna uwekezaji wowote
wa mifugo, majengo na miundombinu uliofanyika katika shamba la Dakawa
ambapo Kampuni ya Sukari ya Mtibwa ilimilikishwa jumla ya hekta 20,000
kwa ajili ya ufugaji wa kisasa kwa muda wa zaidi ya miaka 15 na kwa
upande wa Kitengule na Missenyi kampuni imewekeza ng’ombe 5,307, mbuzi
125 na kondoo 31 ingawa hakuna uwekezaji wowote wa majengo wala
miundombinu kinyume na makubaliano ya mkataba.

Hivyo kufuatia
changamoto hizo, Wizara yake inaandaa madai kwa makampuni hayo ili
yaweze kulipa NARCO fedha yote wanayodaiwa (mapunjo) na pia nimeagiza
makampuni hayo kuwasilisha mpango kazi wa uwekezaji wa miaka mitatu
katika maeneo hayo.

Aidha katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia
 Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) itaendelea kufanya
uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya wanyama; kufanya uhakiki wa ubora
wa vyakula vya mifugo na malighafi za kutengenezea vyakula hivyo, na
kuzalisha na kusambaza dozi milioni 100 za chanjo ya Mdondo,
dozi1,000,000 za chanjo ya Kimeta, dozi 1,000,000 za chanjo ya Chambavu
na dozi 500,000 za chanjo ya ugonjwa wa Kutupa Mimba.

Aidha,
TVLA itakamilisha majaribio na kuanza kuzalisha chanjo dhidi ya ugonjwa
wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe na kuanza majaribio ya kuzalisha chanjo
dhidi ya ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo na chanjo dhidi ya Kichaa
cha Mbwa

Hivyo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara yake
imeliomba Bunge Bunge likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara
 ya Mifugo na Uvuvi ya jumla ya shilingi 56,455,749,000.00.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MPINA AJA NA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
WAZIRI MPINA AJA NA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
https://3.bp.blogspot.com/-nD6EK2Sm8Ng/Wv5v_v5ct_I/AAAAAAAAX2c/620qDhVzVNUTXI94UQjfvnaFGlB1S4PFgCLcBGAs/s640/IMG-20180517-WA0086.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-nD6EK2Sm8Ng/Wv5v_v5ct_I/AAAAAAAAX2c/620qDhVzVNUTXI94UQjfvnaFGlB1S4PFgCLcBGAs/s72-c/IMG-20180517-WA0086.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-mpina-aja-na-mageuzi-makubwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-mpina-aja-na-mageuzi-makubwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy