WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA

Na Rachel Mkundai, Morogoro Jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 17,601 waliokuwa katika sekta isiyo rasmi mkoani Morogoro wamet...




Na Rachel Mkundai, Morogoro

Jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 17,601 waliokuwa katika sekta isiyo rasmi mkoani Morogoro wametambuliwa na hivyo watapatiwa vitambulisho maalumu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.  
Hayo yameelezwa na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu zoezi la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho maalumu wafanyabiashara wadogo wadogo walio katika sekta isiyo rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Masika mjini Morogoro.
Mwandumbya amesema zoezi la utambuzi linafanyika kwa kupitia vikundi vya wafanyabiashara ambapo katika mkoa wa Morogoro vikundi 1851 vyenye jumla ya wanachama 17,601 wametambuliwa na watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye jina na mahali wanapofanyia biashara zao ambavyo watadumu nabyo kwa miaka mitatu.
Ameongeza kuwa kati ya hivyo 1,851, vikundi 473 vimeshapatiwa mafunzo ya umuhimu wa kutambuliwa, kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya TRA, na kati ya hivyo vikundi 143 vyenye jumla ya wanachama 2,324 wameshasajiliwa ili waweze kufanya biashara zao bila usumbufu.
“Lengo ni kuhakikisha kuwa tunawatambua wafanyabiashara wadogo wadogo kwa idadi yao kwa ajili ya serikali kupanga mipango mizuri ya kuboresha biashara zao ziweze kuendelea na vile vile serikali iweze kuweka mipango mizuri ya kuwapatia huduma mbalimbali”, alisema Bw. Mwandumbya.
Akizindua zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe, amesema ulipaji wa kodi ni jambo zuri sana na mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa inayofaidi matunda ya ulipaji kodi kwa kuwa na stendi nzuri ya kisasa ya mabasi ya abiria, stendi ya Msamvu.
“Nitoe rai kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kutumia fursa hii ya kujisajili na kupatiwa vitambulisho vya TRA ili mkoa uweze  kuwapatia huduma muhimu kama vile maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo ndani ya stendi ya Msamvu”, ametoa rai.





Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakishangilia kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa vitambulisho maalum vinavyorasimisha rasmi shughuli zao za biashara mkoani hapo wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (Imeandaliwa Robert Okanda Blogs)


Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Masika mkoani hapo wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa usajili na utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao zoezi ambalo linafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali uliofanyika 21 Mei, 2018 mkoani hapo.


(Juu na chini) Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi pamoja na viongozi wa ngazi ya juu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao 21 Mei, 2018 mkoani hapo.



Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 


Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 


Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (PICHA ZOTE NA TRA)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA
WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF2fzahuqt7yY3kUzweLzSm2Ynw_jBZJeeA0aaCV0s5e2O7Pjr281zCZWifFgOQ8pNg5iXM3htacul_oDIhdhSE7nN0sttotKc3lleQf285pL3LdPhn9FdNsTITkmLamV7Vzi8THcS4p8/s640/PICHA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF2fzahuqt7yY3kUzweLzSm2Ynw_jBZJeeA0aaCV0s5e2O7Pjr281zCZWifFgOQ8pNg5iXM3htacul_oDIhdhSE7nN0sttotKc3lleQf285pL3LdPhn9FdNsTITkmLamV7Vzi8THcS4p8/s72-c/PICHA+1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/wafanyabiashara-wadogo-wadogo-17601.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/wafanyabiashara-wadogo-wadogo-17601.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy