VIDEO;: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAW...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya hima maana Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza kufanya mageuzi makubwa katika eneo la mazingira ya biashara kama ilivyobainishwa hivi karibuni na Waziri wa Viwanda na Biashara.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaotanguliwa na mafunzo endelevu ya Sheria.
“Nawapongeza TAWLA kwa namna ya kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya mafanikio makubwa sana. Nawapongeza  kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu, ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema anatambua na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya sheria.
Mkutano huo wa mwaka huu ambao umebeba  kauli mbiu ya “Uwekezaji Wenye Tija; Kufungua Fursa kwa Mitaji ya Sekta Binafsi na Umma Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi”
Makamu wa Rais amewataka Chama Cha Wanasheria Wanawake wawasaidie wanawake wajasiriamali kujua sheria,  “Sisi kama wanawake kwanza ni kumnyanyua mwanamke, Ukimnyanyua Mwanamke umeinyanyua Tanzania”
Makamu wa Rais aliwahakikishia TAWLA kuwa Serikali haina upungufu wa dhamira. “ Serikali yenu inajali na inao utashi wa kumkomboa mwanamke kiuchumi”
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano maana maslahi ya TAWLA na ya Serikali yanakutana katikati katika suala hili.
Akimkaribisha Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile amewataka TAWLA kutumia maendeleo ya kiteknolojia kujitangaza ili wanawake wengi zaidi wapate taarifa zao na kuweza kupata msaada wa kisheria.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka amesema TAWLA inapenda kuona mtoto wa kike na mwanamke anaendelea kupewa kipaumbele katika maendeleo ya Tanzania.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 













COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIDEO;: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA
VIDEO;: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVhRWsfR0ipz45G84Lb5vZz1GY1TqyFFtXjFrbNMv1ObpTxLGtpe6oBAquRYsVdaDoHX1VECyKp66AcADUVMKa3zOtulEgUOdhKPNHVoDPNiNsmvr7i5Hc8Ud5L7TvaKfO_dDjmYfJD58/s640/4+%252811%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVhRWsfR0ipz45G84Lb5vZz1GY1TqyFFtXjFrbNMv1ObpTxLGtpe6oBAquRYsVdaDoHX1VECyKp66AcADUVMKa3zOtulEgUOdhKPNHVoDPNiNsmvr7i5Hc8Ud5L7TvaKfO_dDjmYfJD58/s72-c/4+%252811%2529.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/video-makamu-wa-rais-afungua-mkutano.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/video-makamu-wa-rais-afungua-mkutano.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy