TSC YAWAONYA WALIMU WANAODANGANYA UMRI WA KUSTAAFU

Na Adili Mhina, Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Rutahindurwa  amewaonya waalimu wanaofanya udangany...



Na Adili Mhina,
Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Rutahindurwa  amewaonya waalimu wanaofanya udanganyifu katika taarifa zao za kiutumishi kwa lengo la kujiongezea muda wa kuwepo katika utumishi wa umma licha ya kuwa umri wao wa kustaafu kwa mujibu wa sheria  umefika.

Rutahindurwa alitoa kauli hiyo jana (Mei 29, 2018) mjini Bagamoyo alipokutana na waalimu wakuu na wakuu wa shule za umma kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kutoa elimu juu ya wajibu wao kama mamlaka ya kwanza ya nidhamu kwa mwalimu kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu na. 25 ya mwaka 2015.
Alieleza kuwa kuna wakati walimu walitakiwa kupeleka taarifa zao za kiutumishi kwa waajiri wao lakini baadhi yao walipeleka taarifa tofauti na zile walizojaza kwenye mikataba ya kazi wakati wa kuanza ajira.
“Kuna baadhi ya waalimu wanajifanya hawakumbuki walizaliwa mwaka gani wakati walijaza mikataba wakati wanaaza ajira na wengi wao wamebadilisha taarifa zao na kujipunguzia umri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria”. Alisema.
Alitoa ufafanuzi kuwa mwalimu atakapoandikiwa kibali cha kustaafu, TSC pamoja na mfuko wamifuko ya hifadhi ya jamii wanajikita zaidi kuangalia taarifa za mwalimu alizojaza awali wakati anaaza ajira yake na sio kutegemea taarifa za stakabadhi ya mishahara peke yake.
Rutahindurwa aliweka bayana kuwa yapo madhara kwa mwalimu ambaye muda wake wa kustaafu utafika lakini akaendelea kuwepo kazini kwa kuwa wakati wa kuchukua mafao yake atakatwa mishahara yote aliyolipwa kwa kipindi chote alichofanya kazi baada ya muda wake wa halali wa kustaafu kupita.
Alisisitiza walimu kuwa,“ naomba muwaeleze waalilmu wote katika shule zenu kuwa utakapoandikiwa kibali cha kustaafu sisi tunaangalia zaidi taarifa zako ulizojaza wakati unaajiriwa na kibainika umedanganya utachukuliwa hatua kwa kuwa umemwibia mwajiri”.
Aliongeza kuwa TSC ina taarifa zote za waalimu walizojaza wakati wakuajiriwa hivyo, kwa waalimu wote ambao hawakumbuki taarifa zao wawasiliane na ofisi za tume ya utumishi wa waalimu katika wilaya zao ili kupata uhakika wa tarehe zao za kustaafu.
Katibu huyo aliwaeleza waalimu kuwa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa walimu namba 25 ya mwaka 2015, wao ndio mamlaka ya kwanza ya nidhamu kwa walimu. Hivyo, wanapaswa kuwashauri na kuwaelimisha waalimu juu ya kanuni na taratibu za kiutumishi badala ya kukaa na kusubiri wafanye makosa ili wawachukulie hatua.
Kwa upande wao waalimu walionesha kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuondoa usumbufu kwa mwalimu pale anafuatilia masuala yake ya mafao mara baada ya kustaafu.
Waalimu hao wametoa pongezi kwa katibu wa TSC kwa jitihada kubwa anazofanya katika kuhakikisha mashauri ya walimu yanafanyiwa kazi  na maamuzi yanatolewa kwa muda muafaka.

Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutahindurwa akiongea na walimu wakuu na wakuu wa shule (hawapo pichani) kutoka Wilaya za Bagamoyo na Chalinze.  Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu, Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Bagamoyo, Happy Kabuka (kulia) akifuatiwa na Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela akiongea katika mkutano wa walimu wakuu na wakuu washule mjini Bagamoyo. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu (kushoto) akifuatiwa na Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutahindurwa pamoja na maofisa wengine walioambatana nao.



Mmoja wa walimu akiuliza swali kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu, Winifrida Rutahindurwa (hayupo pichani) katika mkutano wa walimu wakuu na wakuu wa shule mjini Bagamoyo.


Baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze wakimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutahindurwa (hayupo pichani).

Baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze wakimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutahindurwa (hayupo pichani).

Mmoja wa walimu akiuliza swali kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu, Bibi Winifrida Rutahindurwa (hayupo pichani) katika mkutano wa walimu wakuu na wakuu wa shule mjini Bagamoyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Bibi Fatuma Latu akiongea na Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutahindurwa (kushoto) katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TSC YAWAONYA WALIMU WANAODANGANYA UMRI WA KUSTAAFU
TSC YAWAONYA WALIMU WANAODANGANYA UMRI WA KUSTAAFU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1qGCDqK8uhtVMYbBcvcEOfrFn7bzhmvqSlE2kXYwJFcl5LDr931IaXxNlQRaqE4AP4fUfVdDH4oDsToIolZLRdmq5cRbtAaFkT-bJjNB2YZbgEHqUINR8K-elO7GsNtyCycxsjcMRYOU/s640/01.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1qGCDqK8uhtVMYbBcvcEOfrFn7bzhmvqSlE2kXYwJFcl5LDr931IaXxNlQRaqE4AP4fUfVdDH4oDsToIolZLRdmq5cRbtAaFkT-bJjNB2YZbgEHqUINR8K-elO7GsNtyCycxsjcMRYOU/s72-c/01.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/tsc-yawaonya-walimu-wanaodanganya-umri.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/tsc-yawaonya-walimu-wanaodanganya-umri.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy