SERIKALI INATENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWENYE JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY

 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na m...







 WAZIRI
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano
kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga

 Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa
halfa hiyo kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu kushoto  ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS)
Faidha Salimu

 Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza kwenye halfa
hiyo kushoto  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo

 Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akifungua mlango mara baada ya kuzindua  madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akingia ndani ya madarasa mara baada ya kuyazindua kulia ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi

 Mkurugenzi
wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia akimuonyesha kitu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kabla ya
kuzindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi

 Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia
akifurahia jambo na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa
Selebosi mara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya msingi Bombo

 Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio mbalimbali





 Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa
kwenye picha akiwa amekalia madawati mara baada ya kufanya uzinduzi huo



Kundi la Wasanii la Tanga Kwanza likitumbuiza kwenye uzinduzi huo

Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa
kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua madarasa hayo kushoto ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kulia mwenye
suti ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimukatika
akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Bombo



Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wanaounda kundi la Tanga Kwanza





WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni
55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo
kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.



Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11
kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi
wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje
ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana
na mapato ya ndani.



Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule
ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao
uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.



Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi
cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili
kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili
kupitia sekta hiyo.



“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo
yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila
kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali
inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi
kushirikiana nanyi”Alisema.



“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha
hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi
wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa
watoto wetu elimu bora “Alisema.



Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279
zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.



Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John
Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia
kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio
wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.



“Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa
kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana
na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema
tutaendelea kushirikiana”Alisema.



Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi
aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa
kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili
wananfunzi waweze kuendelea na masomo.



“Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa
msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa
wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha
kutokupata matokeo mazuri “Alisema. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha )

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI INATENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWENYE JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
SERIKALI INATENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWENYE JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpvWXEOR36nAHXNWLx9wkpAfzoT2MvT1AGbvdAQjBRN8RJ8c-pxv9rlmA7UZFNUF4ByYrKTsrq1usmCBlza0PEkpsfWECBIBytzPOlWYwsULsZMLzjBZPpxos_xwaDH_jlfDACxPW-w68/s640/_MG_4515.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpvWXEOR36nAHXNWLx9wkpAfzoT2MvT1AGbvdAQjBRN8RJ8c-pxv9rlmA7UZFNUF4ByYrKTsrq1usmCBlza0PEkpsfWECBIBytzPOlWYwsULsZMLzjBZPpxos_xwaDH_jlfDACxPW-w68/s72-c/_MG_4515.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/serikali-inatenga-kila-mwezi-milioni-55.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/serikali-inatenga-kila-mwezi-milioni-55.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy