MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa k...



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi Mdogo wa ofisi ya Mkoa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akiitoa katika uzinduzi rasmi wa kamati hiyo.
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wakuu wa wilaya za Siha, Onesmo Buswelu (kushoto)  ,Wilaya ya Same Rosemery Senyamule (katikati) na Aron Mbogho wa wilaya ya Mwanga wakiwa katika kikao hicho ambao wao pia ni wajumbe  
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa huo.
Mkuu wa wilaya ya Siha,Onesmo Buswelu akichangia jambo wakati wa kikao hicho cha uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro iliyozinduliwa rasmi .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .





serikali mkoani
Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala
ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za
kisekta za serikali za mitaa.







Mbali na majukumu
hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya
usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali
katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za
mkoa kwa kushirikiana na wakala.







Akizindua kamati
hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za
kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa
kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na
kuwajibika ipasavyo.







“Sheria hii
inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa
imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia
tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa
“alisema Mghwira.







Mghwira alitoa
maelekzo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kamati za maafa za wilaya, kata na
vijiji zinaundwa na kusimamiwa ili zitekeleze majukumu yake ipasavyo kwa mujibu
wa sheria hiyo huku akiwaagiza wakulurugenzi kuwawezesha wakuu wa wilaya
kuandaa utaratibu wa kutoa maelekezo kwa kamati a wilaya ,kata na vijiji .







“Hakuna haja ya
kusubiri maafa yatokee ndiyo tufanye maandalizi ,tuanze sasa,kwa taarifa
nilizonazo mvua bado zinaendelea ,twendeni katika maeneo yanayotuzunguka kutoa
tahadhari za awali kwa wananchi wote wanaooonekana kupata madhara kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha”alisema Mghwira.



                                            









COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6PTZjdf2CcPE1UiPr3zuM0NelseGTbcCjD2mlmwHPy_u1fH1HHSbiTRcK1XcxDpVlEVkCQ3F0FGbkQXghLoO0CSCO924R-FWbpv76EVySTmp1Sv0idBKknUxR4weIHG5MsxXowUHiNF-N/s640/_MG_7688.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6PTZjdf2CcPE1UiPr3zuM0NelseGTbcCjD2mlmwHPy_u1fH1HHSbiTRcK1XcxDpVlEVkCQ3F0FGbkQXghLoO0CSCO924R-FWbpv76EVySTmp1Sv0idBKknUxR4weIHG5MsxXowUHiNF-N/s72-c/_MG_7688.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/mkuu-wa-mkoa-wa-kilimanjaro-azindua.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/mkuu-wa-mkoa-wa-kilimanjaro-azindua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy