TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika akisisitiza kuhusu sheria inayotumika kutoa likizo kwa watumishi katika sekta ya umma na binafsi pale wanapojifungua. PIX2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha makazi ya Askari Polisi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX3. Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX4. Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo. PIX5. Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA...


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kusimamia usafiri wa anga kwa kuzingatia taratibu na kanuni za usafiri huo ili kuweka uwiano wa haki kwa waendeshaji na abiria wanaotumia usafiri huo.
Ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizindua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuwapongeza kwa kuamua kuweka mikakati ya kununua rada nne kwa kutumia fedha za ndani.
“Lazima msimamie kanuni na taratibu zilizopo, wajibu wenu ni kutoa haki kwa watumiaji na abiria kwa usawa, hatutaki kusikia mnakandamiza watumiaji wa usafiri na mkisimamia vizuri eneo hili mtafanya idadi ya watumiaji kuongezeka na makampuni kuendelea kuwekeza zaidi kwenye usafiri” amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amesema yeyote anaevunja taratibu zilizowekwa kwenye usafiri wa anga Mamlaka hiyo ichukue hatua stahiki kulingana na taratibu zilizopo ili usafiri huo uweze kuwa na nidhamu.
“Kila Kampuni mkiiachia ifanye inavyotaka hatutafika popote na malalamiko kwenye usafiri wa anga yataendelea kuwepo, hivyo naomba msimamie makampuni haya kwa ukaribu mkubwa,’ amesisitiza Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa ili mamlaka ifikie lengo na kufanikiwa lazima Menejimenti ishirikishe watumishi kwa karibu ili kutimiza malengo iliyojiwekea.
Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa TCAA kuwawezesha watumishi wake kitaaluma na kimaslahi ili kuongeza tija katika kazi na kufikia malengo ya utendaji Kitaifa na Kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw, Hamza Johari, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa TCAA imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia vyanzo vya ndani ili kuvutia makampuni ya ndege ya ndani na nje ya nchi.
“Nikuhakikishie kuwa tumejipanga kutekeleza miradi mingi zaidi kwenye usafiri wa ndani ili kuchochea kasi ya usafiri huo lakini pia kutimiza amza ya kuboresha usafiri huo, ”amesema Johari.
Ameongeza kuwa kwa sasa mamlaka iko kwenye hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa kufunga vifaa maalum vya kuwezesha ndege kwa usalama katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar ambapo mradi huo ukikamilika utaimarisha huduma za kuongozea ndege katika kiwanja  hicho.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI, MAWASILIANO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, mjini Dodoma.




Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, lililofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimkabidhi  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari nyaraka mbalimbali mara baada ya kulifungua mjini Dodoma.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) lililofanyika mjini Dodoma. 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika akisisitiza kuhusu sheria inayotumika kutoa likizo kwa watumishi katika sekta ya umma na binafsi pale wanapojifungua. PIX2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha makazi ya Askari Polisi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX3. Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX4. Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo. PIX5. Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika akisisitiza kuhusu sheria inayotumika kutoa likizo kwa watumishi katika sekta ya umma na binafsi pale wanapojifungua. PIX2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha makazi ya Askari Polisi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX3. Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX4. Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo. PIX5. Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpiU4zepNxWDfpXUpmClTLyXZhGLxGGMQPBF8qc7obWxgU22TIenOqPtHNrQLjGPYTr3oOOmXtUsxrn1-fBuZGn4LkE_GcvHrVyPJhni5NZlEbUtCm0jz5_28NcFmqq8XYh6LDN3v1CyA/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpiU4zepNxWDfpXUpmClTLyXZhGLxGGMQPBF8qc7obWxgU22TIenOqPtHNrQLjGPYTr3oOOmXtUsxrn1-fBuZGn4LkE_GcvHrVyPJhni5NZlEbUtCm0jz5_28NcFmqq8XYh6LDN3v1CyA/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/tcaa-yaagizwa-kusimamia-usafiri-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/tcaa-yaagizwa-kusimamia-usafiri-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy