MPRU YAPATA MTENDAJI MPYA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Kutathmini U...




Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina(aliyekaa katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Kutathmini Utendaji wa
Sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria baada ya kukabidhi taarifa hiyo
mjini Dodoma hivi karibuni.Waliokaa kuanzia kushoto Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Mhandisi Bonaventure Baya Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi, Dk Yohana Budeba, aliyesimama kuanzia
kushoto John Komakoma Kaimu Meneja wa MPRU.
Na John Mapepele, Dodoma



Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina amemteua John
David Komakoma kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Hifadhi ya Bahari na
Maeneo Tengefu nchini (MPRU) baada ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa
awali Dkt. Milali Machumu kutokana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali kubaini dosari katika usimamizi wa Kitengo hicho.



Pia Waziri Mpina amevunja Bodi ya Wadhamini ya MPRU iliyokuwa chini ya
Uenyekiti wa Profesa John Machiwa ambayo ilikuwa na Wajumbe nane.



Mpina alisema ameamua kuvunja bodi na kumsimamisha Mtendaji huyo kwa
mamlaka aliyonayo kulingana na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo
Tengefu, Na 29 ya mwaka 1994.



Aidha Mpina amemwagiza Katibu Mkuu wa Uvuvi kuunda Kamati ya
kuchunguza utendaji wa kazi wa Mtendaji wa awali.



Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Komakoma ambaye ni mtaalam wa
Bailojia ya Baharini amesema atahakikisha kuwa maeneo yote ya bahari
yaliyotengwa yanahifadhiwa kikamilifu ili kuleta Mchango mkubwa katika
taifa letu.



“Nina imani kwamba maeneo haya ni muhimu sana kwa uhifadhi wa
raslimali za bahari na utalii endelevu hivyo hatuna budi kuyasimamia kwa
faida ya sasa na vizazi vijavyo” alisisitiza Komakoma.



Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kiliundwa na sheria ya
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu  Mwaka 1994 ambapo baadhi ya
majukumu yake makuu yameanishwa katika sehemu ya VI kifungu cha 10
ambayo ni pamoja na kulinda na kuhifadhi maeneo yenye mkusanyiko mkubwa
wa bioanuai pamoja na mifumo ya ikolojia ya baharini na mwambao wa
pwani.



Kuhamasisha wananchi kutumia kwa busara raslimali ambazo hazitumiki
kabisa au hazitumiki kikamilifu kwa sasa, kusimamia maeneo ya bahari na
mwambao wa pwani ili kuwezesha matumizi endelevu ya raslimali na
ukarabati wa maeneo yaliyoharibiwa.



Kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi wanashirikishwa
katika nyanja zote za upangaji,uendelezaji na usimamizi wa raslimali.



Hadi sasa kuna Hifadhi za Bahari tatu na Maeneo Tengefu 15 hapa
nchini katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Mtwara.



Kabla ya uteuzi huu Komakoma alikuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi
Msaidizi wa Uvuvi katika Kitengo cha Udhibiti Ubora, Usalama, Viwango na
Masoko ya Mazao ya Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MPRU YAPATA MTENDAJI MPYA
MPRU YAPATA MTENDAJI MPYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSZcSBk-SBF9SclXRwTanokFTiX-S6SfjhID-Eprs8aa0pGEtN3UKjklhtLdt4GFI_jhyleRPnUPPylXZY4a7iawiYns7yWTZ3GUW8dphNUmsDDSnwQ1z8PlZQ-63-fM2XxRAE35Sa6Mc/s640/a%25281%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSZcSBk-SBF9SclXRwTanokFTiX-S6SfjhID-Eprs8aa0pGEtN3UKjklhtLdt4GFI_jhyleRPnUPPylXZY4a7iawiYns7yWTZ3GUW8dphNUmsDDSnwQ1z8PlZQ-63-fM2XxRAE35Sa6Mc/s72-c/a%25281%2529.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mpru-yapata-mtendaji-mpya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mpru-yapata-mtendaji-mpya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy