HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IDARA YA HABARI-MAELEZO          TAARIFA KWA UMMA HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA K...







JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

IDARA YA HABARI-MAELEZO

        



TAARIFA KWA UMMA
HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA
Dodoma, April 18, 2018:

Upatikanaji wa maji mijini na vijijini umeimarika kutoka chini ya 50% ya awali kutokana na umakini katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji safi nchini. Aidha, ili kukabiliana na mazingira Serikali imeanza mchakato wa kutumia mifumo ya kisayansi ili kuondoa matumizi ya mkaa majumbani.

Hatua hizo zimebainishwa leo na Mhe. Isack Kamwelwe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira) walipokuwa wakieleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.

Akizungumzia hoja kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji nchini, Waziri Kamwelwe amesisitiza kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, ufuatiliaji na kuzibwa mianya ya ubadhirifu vimeleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini.

“Sisi kwa upande wetu CAG anatuonesha njia ili tufanye vizuri zaidi. Hadi kufikia Desemba, 2017, upatikanaji wa maji mijini umepanda hadi kufikia asilimia 78. Kwa upande wa vijijini, hadi kufikia Machi 2018, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imejenga vituo vya kuchotea maji 123,888 vyenye uwezo wa kuhudumia takribani watu milioni 30 sawa na asilimia 68.8,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri Makamba amesema hoja za CAG zimewasaidia kuongeza mikakati hasa ya kutumia sayansi na teknolojia kupata mbadala wa matumizi ya mkaa ili kuokoa misitu na kutunza mazingira. Amesema tayari Ofisi yake na wadau wanafanya majaribio ya baadhi ya teknolojia hizo.

Kuhusu changamoto za kupambana na taka za kielektroniki, amekiri kuwa Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea inakumbana na changamoto ya kupokea vifaa vingi vilivyotumika kama kompyuta, simu na chaja ambavyo huharabika haraka na kutupwa kama taka za kielectroniki.

“Ofisi ya Makamu wa Rais imeanza kutoa vibali kwa makampuni 16 yenye utaalamu kwa ajili ya kukusanya, kusafirisha na kurejeresha (recycling) taka za kielektroniki,” alisema.  

Imetolewa na:



Dkt. Hassan Abbasi,
Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.



Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  katika Wizara yake mapema leo mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu hoja mbalimnbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Ofisi hiyo mapema leo mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Mawaziri wote kukutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika  ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Wizara zao mapema leo mjini Dodoma.











COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA
HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA
https://lh4.googleusercontent.com/A4mchLAsv4WKJ3FFYj4FmJF4YL6yFV_WDWKaQy5VqbUt6-LVamz88TUeNf-GFLjdDToNWqJqao9IccJJQAcJOGpEHCnsGrrjy5-mxFJi1vtyDNQnqlTFU3FPNdVe2hX2-S5g93lThUW3p5rdSQ
https://lh4.googleusercontent.com/A4mchLAsv4WKJ3FFYj4FmJF4YL6yFV_WDWKaQy5VqbUt6-LVamz88TUeNf-GFLjdDToNWqJqao9IccJJQAcJOGpEHCnsGrrjy5-mxFJi1vtyDNQnqlTFU3FPNdVe2hX2-S5g93lThUW3p5rdSQ=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/huduma-za-maji-zaimarika-teknolojia.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/huduma-za-maji-zaimarika-teknolojia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy