MNEC MWAKA RAMADHAN AMEVUNA WANACHAMA WAPYA (80) KATA YA MKWAWA MANISPAA YA IRINGA

  Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiongea n...



 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiongea na wanawake waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza kwenye ziara ya UWT taifa mkoani Iringa katika Kata ya Mkwawa.

Baadhi ya wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT katika kata ya Mkwawa wakatika wa ziara ya viongozi wa kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa katika kitendo cha kula kiapo pamoja na wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT kata ya Mkwawa
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo Pamoja katibu wa UWT manispaa ya Iringa


Na Fredy Mgunda, Iringa

MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan amevuna wanachama wapya zaidi ya themanini (80) katika kata ya Mkwawa Manispaa ya
Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.



Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo MNEC Ramadhan alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa kata ya Mkwawa ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa MNEC huyo.



Ramadhan alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama
ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia
mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu
katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.



“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisema Ramadhan



Aidha Ramadhan aliwataka wanawake kujifunza
kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.



“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama
sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisema Ramadhan



Ramadhan alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa
maendeleo yako.



“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha
hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Ramadhan



Ramadhan alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya
Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.



“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona
faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Ramadhan



Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.



“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali
mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Kabati


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MNEC MWAKA RAMADHAN AMEVUNA WANACHAMA WAPYA (80) KATA YA MKWAWA MANISPAA YA IRINGA
MNEC MWAKA RAMADHAN AMEVUNA WANACHAMA WAPYA (80) KATA YA MKWAWA MANISPAA YA IRINGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiN74YmeqaVOIEaPuAV-ClfITtXBwstFnsgtI-E1DeMLo-mkduBNyMAnp4T03Q4qwRQeVSPAcnSLfNUB8KhynCp_0hhddE6ZO8h-ajVAVORbumbAZAFs__413fYBvUS5_dqMlXC7L4DWLSF/s640/IMG_1014.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiN74YmeqaVOIEaPuAV-ClfITtXBwstFnsgtI-E1DeMLo-mkduBNyMAnp4T03Q4qwRQeVSPAcnSLfNUB8KhynCp_0hhddE6ZO8h-ajVAVORbumbAZAFs__413fYBvUS5_dqMlXC7L4DWLSF/s72-c/IMG_1014.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mnec-mwaka-ramadhan-amevuna-wanachama.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mnec-mwaka-ramadhan-amevuna-wanachama.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy