UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI.

Serikali  imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya ...



Serikali  imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara hiyo.

Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 117.9 na utachukua miezi 24 mpaka kukamilika kwake.

"Serikali imeanza rasmi ujenzi wa barabara hii na sasa ni jukumu lenu kuhakikisha mnampa ushirikiano mkandarasi huyu ili mradi uwahi kukamilika mapema", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani.

Ameongeza kuwa sasa Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka daraja la Kikwete mpaka Uvinza, mkoani Kigoma na hivyo itasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi kutoka mkoa wa Dar es Salaam mpaka mikoa ya katavi na Kigoma kupita kwenye lami njia nzima.

Naye Mbunge wa Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa yeye na timu yake watajitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutohujumu vifaa vya mkandarasi huyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi, ameishukuru Serikali kwa mradi unaoendelea katika wilaya hiyo na kumuahidi Waziri kuwa yeye na kamati ya usalama itahakikisha mkandarasi hahujumiwi.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi DamianNdibalinze, amemueleza Waziri kuwa kazi imeanza kwani Mkandarasi ameshaanza kuleta vifaa eneo la kazi na ujenzi wa kambi unaendelea.

Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea mkoani humo.
Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO kutoka China, Bw. Li, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiwaonesha Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi na Mbunge wa Jimbo la Igalula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami itajengwa, mkoani Tabora.


Tingatinga likikata miti kwa ajili ya kusafisha eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami utaanza, mkoani Tabora. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI.
UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkpoaft76D3pK8lIOhGXAYCia9RgIL8v9k5nI16Ntuyf3hYR7Sfskam2isH0TzxbzUV7vzw6G8cLp1CecRAREJ3-Lrx5cMnuNqCyrQclhE157Jdv_OI0lyKhFsrZorF5_3RI9JfmZg46I/s640/1+%25286%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkpoaft76D3pK8lIOhGXAYCia9RgIL8v9k5nI16Ntuyf3hYR7Sfskam2isH0TzxbzUV7vzw6G8cLp1CecRAREJ3-Lrx5cMnuNqCyrQclhE157Jdv_OI0lyKhFsrZorF5_3RI9JfmZg46I/s72-c/1+%25286%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/ujenzi-wa-barabara-ya-nyahua-chaya-km.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/ujenzi-wa-barabara-ya-nyahua-chaya-km.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy