NDITIYE: BANDARI ITOE NAFASI YA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANACHUO

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimtunu...




Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimtunuku cheti kwa kufaulu vizuri masomo yake mmoja wa wahitimu Bi. Shekha Habibu Humudi wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam yaliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Joseph Kakeneno na wa kwanza kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga


Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga akimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari ya Dar es Salaam Prof. Ignas Rubalatuka, akiwaasa wahitimu (hawapo pichani) wa chuo hicho wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wahitimu, wanachuo, wafanyakazi, wageni waalikwa na wazazi (hawapo pichani) kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam yalyofanyika chuoni hapo Dar es Salaam

NA WUUM

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na uongozi wa Menejimenti wa Mamlaka hiyo kutoa nafasi kwa wanachuo wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kufanya mafunzo kwa vitendo wakati wa masomo yao kwenye bandari zote nchini.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Bar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 521 wametunikiwa cheti cha kuhitimu mafunzo yao katika ngazi ya elimu ya astashahada na stashahada ya mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo ya usimamizi wa shughuli za meli na bandari; uhandisi na usimamizi wa matengenezo; zimamoto na usalama; masoko na mawasiliano ya umma; usimamizi wa wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo; usimamizi wa mipango ya uchukuzi na usafirishaji; na utawala na biashara.

Ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha bandari zetu, kuongeza ufanisi na tija katika utendaji kazi wa sekta ya usafirishaji majini ili kukuza uchumi na kuongeza mapato la taifa letu.

Pia, wakati akisoma hotuba yake kwa wahitimu hao, Mhandisi Nditiye amewataka wahitimu hao kutumia vyeti vyao na taaluma waliyoipata vizuri kwa kukitangaza vema Chuo cha Bandari Dar es Salaam aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa ndani na nje ya nchi. Aidha, amesisitiza kuwa wanaoajiriwa kuwa wafanyakazi wa bandari mbalimbali wawe wamehitimu chuo na kuwa na elimu inayotakiwa. Vile vile amemuagiza Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt. Joseph R. Kakeneno kujenga zahanati kwa ajili ya kutoa huduma za tiba kwa wanachuo na jamii ya Chuo hicho.

Naye mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa bodi wa Mamlaka hiyo Prof. Ignas Rubalatuka, katika mahafali hayo amewataka wanachuo kusoma kwa bidii ili waweze kuajiriwa na kufanya kazi mahali popote iwe ndani au nje ya nchi.

Aidha, wahitimu wa chuo hicho wamemshukuru Dkt. Kakeneno kwa kufanikisha upatikanaji wa ithibati sita za kozi mbalimbali kati ya ithibati nane zinazohitajika. Hivyo, wamemuomba mgeni rasmi Mhandisi Nditiye kumsaidia Dkt. Kakeneno kupata ithibati nyingine mbili zilizosalia.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Nditiye ametoa mwezi mmoja kwa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kurudisha majengo ya Chuo hicho, uwanja wa michezo na mali zote zilizokuwa zinatumiwa na Chuo cha Hoteli na Utalii ambazo ziko ndani ya eneo la Chuo cha Bandari ya Dar es Salaam yarudishwe kwenye Chuo cha Bandari.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama) akiwatunuku vyeti wahitimu 529 (hawapo pichani) wa astashahada na stashahada wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kwenye mahafali ya 16 ya Chuo hicho yaliyofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam




Mgeni rasmi wa Mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Chuo hicho. Aliyeketi wa kwanza kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Joseph Kakeneno


Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam Bi. Nuru Mhando (wa kwanza kulia) akimkaribisha mgeni rasmi wa Mahafali ya 16 ya Chuo hicho Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) alipowasili chuoni hapo. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Joseph Kakeneno

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NDITIYE: BANDARI ITOE NAFASI YA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANACHUO
NDITIYE: BANDARI ITOE NAFASI YA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANACHUO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipDvo8t4D_R1Fcokvd0Gy5TIccEJGyBaQl3wZfwAWyWYmK0BY_CM837mSVeY7f-CNsaRx0p7klFGk9eXA7a4Hxit04HPJXbMmwlh9cuN3Q3LfReP0Xg4OGizNxy5NiCizuX4XmCVS45JP_/s640/JPEG.+NA.+4.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipDvo8t4D_R1Fcokvd0Gy5TIccEJGyBaQl3wZfwAWyWYmK0BY_CM837mSVeY7f-CNsaRx0p7klFGk9eXA7a4Hxit04HPJXbMmwlh9cuN3Q3LfReP0Xg4OGizNxy5NiCizuX4XmCVS45JP_/s72-c/JPEG.+NA.+4.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/nditiye-bandari-itoe-nafasi-ya-mafunzo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/nditiye-bandari-itoe-nafasi-ya-mafunzo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy