F MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIONGOZI KTOVUMILIA WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI-SIMIYU | Okandablogs

Wednesday, February 21, 2018

MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIONGOZI KTOVUMILIA WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI-SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa na wilaya mkoani Simiyu kusimamia sheria na kutowafumbia macho wanaowapa mimba wanafunzi.
Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwandoya Kisesa, wilayani Meatu.
Makamu wa Rais alisema “Jamani mnadhulumu watoto wetu hapa kuna kina Samia wa baadae mnapokuja kuwapa ujauzito mapema mkawavunjia safari zao, mkawaoa mapema, wakina Samia hawataibuka Meatu, tutatoka huko nje tutaibuka hapa Meatu, tunataka Samia atoke hapa Meatu waachieni wasome, masuala ya mimba za utotoni wapunguzieni.”
Makamu wa Rais aliwahimiza wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye mifuko ya bima ya afya kwani inafaida kubwa sana.
“Magonjwa yaweza kukufika wakati huna pesa na kitu pekee kitakachokusaidia ni bima yako ya afya hivyo wananchi hakikisheni mnapovuna na kuuza mazao yenu mnapata bima ya afya”
Makamu wa Rais aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa kulima pamba kwa wingi ambapo wilaya hiyo inategemea kilo 84 na kuwaahidi wananchi hao kuwa dawa za kuulia wadudu zitapatikana kwa wingi kuanzia mwisho wa mwezi huu kwani serikali imetoa fedha zaidi ya bilioni 9 .
Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa barabara zote ambazo ilani ya uchaguzi imeahidi kuzijenga zitajengwa na zile ambazo hazipo kwenye ilani ila zina umuhimu zitaingizwa kwenye bajeti ijayo.
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luaga Mpina alisema kuwa kati ya kata 13 ni vijiji vine tu vina maji hivyo alimuomba Waziri wa Maji kusaidia zaidi upatikanaji wa maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe aliahidi kusimamia kwa ukamilifu upatikanaji wa maji .

0 comments:

Post a Comment