WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya matibabu ya bure kwa wazee, Johaness Chacha, moja wa wazee 280waliopatiwa vitambulishbo hiv...




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya matibabu ya bure kwa wazee, Johaness Chacha, moja wa wazee 280waliopatiwa vitambulishbo hivyo vitakavyowawezesha kutibiwa bure popote wilayani Serengeti katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya Mugumu Januari 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


AZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60.

Waziri Mkuu alikabidhi kadi hizo jana (Alhamisi, Januari 18, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, inayojengwa katika mji wa Mugumu.Alisema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti itakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo, itakayokuwa na uwezo wa kuwahudumia wakazi wa wilaya hiyo na wageni.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu kwa kuwa mbali na kuwanufaisha wananchi, pia watalii wanaotembelea mbuga ya Serengeti nao wataweza kutibiwa hapo.Awali, Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Nurdin Babu alisema tangu mwaka 1974 wilaya hiyo ilipoanzishwa hadi sasa haina hospitali ya wilaya na wakazi wake wanatibiwa katika hospitali teule ya Nyerere inayomilikiwa na kanisa la Mennonite Tanzania.

Alisema kutokana na kuongeka kwa idadi ya wakazi hao pamoja na idadi kubwa ya wageni wanaotembelea Serengeti, hususan watalii hospitali hiyo haina tena uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kinachostahili.Bw. Babu alisema mara nyingi wageni wanaotembelea mbuga ya Serengeti hulazimika kufuata huduma za afya mjini Arusha au Nairobi nchini Kenya pale wanapougua au kupata ajali katika shughuli zao za kitalii.

Alisema kwa upande wa wakazi wa wilaya ya Serengeti wao hulazimika kufuata huduma za afya katika hospitali ya Mkoa au hospitali ya Rufaa ya Bugando, hivyo kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa hospitali utawapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Pia Mkuu huyo wa wilaya alisema alianzisha kampeni ya changia sh. 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya, kwa lengo la kuwafanya wakazi hao wajisikie kuwa wameshiriki katika ujenzi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 19, 2018.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280
WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkpR1gAUFkBP9M9SnpNZYbusabjuH4iF6EvlhWoCX01LM3TNeHXg6R7dTVbTwWdWPWYz-8eNt9wr-KrouZ8MMOdhuU_2AJ9oXYtPsDptkm0ixfgOkPM-jSwGI9IBtdL9m49hwVgViYKo_z/s640/PMO_9013.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkpR1gAUFkBP9M9SnpNZYbusabjuH4iF6EvlhWoCX01LM3TNeHXg6R7dTVbTwWdWPWYz-8eNt9wr-KrouZ8MMOdhuU_2AJ9oXYtPsDptkm0ixfgOkPM-jSwGI9IBtdL9m49hwVgViYKo_z/s72-c/PMO_9013.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-akabidhi-kadi-za-matibabu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-akabidhi-kadi-za-matibabu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy