VYOMBO VYA HABARI VYAASWA KUZINGATIA MAADILI

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari ...


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.
"Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa" amefafanua Dkt. Abbasi.
Aidha, Dkt. Abbasi ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.
“Mkiwa kama Kampuni ya Magazeti ya Serikali mnatakiwa kuibeba agenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda" ameongeza Dkt.Abbasi.
Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita katika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.
Aidha, Dkt. Abbasi amesisitiza umuhimu wa wanataaluma ya habari kujiendeleza kitaaluma ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, mwandishi wa habari atatakiwa kuwa na  atashahada ya taaluma ya uandishi wa habari.
Akizungumzia kuhusu upatkanaji wa habari, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imewekeka mfumo wa kisheria kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara na Taasisi zake.
Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesisitiza waandishi wa habari kujisajili ili wapatiwe vitambulisho (Press Card) kwani kuanzia mwezi Machi mwaka huu katika matukio yote ya viongozi wakuu wa Kitaifa,  kila mwanahabari atatakiwa kuwa na kitambulisho hicho.

Muwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Mkoani Dodoma Bw. Felix Mushi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika Ofisi za Kampuni hiyo Mkoani Dodoma.
.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaeleza watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) umuhimu wa kubeba  ajenda ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda wakati wa ziara yakutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma  iliyoanza mapema leo.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Kampuni ya                         Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutembelea Ofisi hizo mapema leo ili kujionea utendaji wa Kampuni hiyo na Kusisitiza uzingatiaji wa maadili ya uandishi  wa habari.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiagana na watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoani Dodoma mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Kampuni hiyo mapema leo.



Watumishi wa Gazeti la Mwananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma iliyoanza Januari 17, 2017.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Mkoani Dodoma mara baada  ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo  na kuzungumza na wafanyakazi, kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Gazeti la Mwananchi.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VYOMBO VYA HABARI VYAASWA KUZINGATIA MAADILI
VYOMBO VYA HABARI VYAASWA KUZINGATIA MAADILI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAazKYBjQmh44MiP3pO1SfDzwYuRxr1NkgYxtEhpm9EpelxUWgBPF0MSOMnUx4oW_1jAPsEZjXaVTZNh_VU8HYNMns0bpc1NhnqO9URHb440B4szOUUGNS4MnQu2S1n-7ltzUG2VxVcl0/s640/6945.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAazKYBjQmh44MiP3pO1SfDzwYuRxr1NkgYxtEhpm9EpelxUWgBPF0MSOMnUx4oW_1jAPsEZjXaVTZNh_VU8HYNMns0bpc1NhnqO9URHb440B4szOUUGNS4MnQu2S1n-7ltzUG2VxVcl0/s72-c/6945.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/vyombo-vya-habari-vyaaswa-kuzingatia.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/vyombo-vya-habari-vyaaswa-kuzingatia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy