RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU NA TAMISEMI, APIGA MARUFUKU MICHANGO MASHULENI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz T...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuchukuliwa hatua dhidi ya viongozi na watendaji ambao shule za msingi na sekondari zilizopo katika maeneo yao zinawatoza wanafunzi michango mbalimbali kinyume na muongozo uliotolewa na Serikali wa utoaji wa elimu bila malipo.
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 17 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Lazaro Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Said Jafo.
Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inatoa Shilingi Bilioni 23.875 kila mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo lakini inashangaza kuona bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao wanashindwa kutoa michango hiyo.
“Nawaagiza Mawaziri, sitaki kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kutoa michango, na fikisheni maagizo haya kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wote wanaohusika, nikisikia tena mahali jambo hili linaendelea hawa niliowateua mimi wataondoka.
“Haiwezekani tumefuta ada, halafu walimu wanaamua kuanzisha michango tena mikubwa ambayo watu masikini wanashindwa kusomesha watoto wao, na kama wazazi wanataka kuchangia kitu shuleni wapeleke michango yao kwa Mkurugenzi, lakini sitaki kusikia mwanafunzi anapewa sharti la kutoa mchango ndipo apokelewe shule” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo baadhi ya shule ambazo wanafunzi wanadaiwa michango mbalimbali tena kwa kiwango kikubwa ikiwemo chakula, maabara, madawati na ziara za kujifunza, hali iliyosababisha wazazi kushindwa kumudu.
Waziri Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ameagiza walimu na viongozi wa halmashauri kuwarudisha shule mara moja wanafunzi wote waliorudishwa nyumbani kwa kutotoa michango na pia kurejesha mara moja michango iliyokusanywa kinyume na mwongozo wa Serikali.
Waziri Mhe. Selemani Said Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya shule ambazo zimetoza michango kinyume na mwongozo wa Serikali ifikapo Ijumaa wiki hii (tarehe 19 Januari, 2018) ili hatua zichuliwe dhidi ya walimu na maafisa elimu ambao kwa makusudi wamekiuka mwongozo huo.  


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Januari, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. Taarifa kamili inakuja. (Picha na IKULU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ktika picha ya pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018, baada ya kufanya nao mazungumzo. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. Taarifa kamili inakuja. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari baada ya kufanya mzungumzo na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 17, 2018. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari baada ya kufanya mzungumzo na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 17, 2018. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari baada ya kufanya mzungumzo na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 17, 2018. 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU NA TAMISEMI, APIGA MARUFUKU MICHANGO MASHULENI
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU NA TAMISEMI, APIGA MARUFUKU MICHANGO MASHULENI
https://lh3.googleusercontent.com/nW24vL4RdoYxkHqbdf2Hy0b3oxC2juezX51MHEp3Idw2qpZwbLQlmSHKz7AD6ugIZzQ31_dcmwLiRq7lZQ_CVSAXur8RY3ug0dZlWd-okxo05NtSTGYaiINZ9VP-fYFb22_tcvevYl97Q3Lg_g
https://lh3.googleusercontent.com/nW24vL4RdoYxkHqbdf2Hy0b3oxC2juezX51MHEp3Idw2qpZwbLQlmSHKz7AD6ugIZzQ31_dcmwLiRq7lZQ_CVSAXur8RY3ug0dZlWd-okxo05NtSTGYaiINZ9VP-fYFb22_tcvevYl97Q3Lg_g=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-akutana-na-mawaziri.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-akutana-na-mawaziri.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy