WAZIRI MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI

Na Benny Mwaipaja, Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjin...


Na Benny Mwaipaja, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjini Dodoma na kutoa wito kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Amesema hayo baada ya kushuhudia mkandarasi anayejenga jengo hilo Hainan International Ltd ya China, akitumia vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyopatikana hapa nchini zikiwemo mbao na vifaa vya umeme, hatua ambayo amesema inachangia kuwaongezea kipato wananchi.

Akizungumzia ujenzi huo, Dkt. Mpango amesema jengo hilo litatumika ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwakuwa litatumika kuchakata takwimu mbalimbali zitakazotumika katika kutunga sera na mipango mbalimbali ya kuendeleza nchi.

“Huwezi kupanga mipango yoyote bila kuwa na takwimu nzuri na bora, hapa ndipo vile “vichwa” vyetu vya takwimu nchini vitachakata takwimu hizo ndipo zitumike katika kutunga sera bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu” Alisistiza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alielezea furaha yake kwamba jengo hilo linajengwa mjini Dodoma badala ya Dar es Salaam ambako lilikuwa lijengwe ili kusukuma azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma kwa kuhakikisha miundombinu muhimu zikiwemo ofisi vinapatikana.

Aidha, ameeleza kuwa ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa 5, umetoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 kutoka sehemu mbalimbali nchini hatua ambayo amesema imewafanya vijana wengi kujipatia kipato cha kujikimu maisha yao.

Dkt. Mpango ameupongeza uongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kwa kazi nzuri wanayoifanya ya ujenzi wa ofisi mpya katika Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma inayojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa ya Canada na Uingereza kwa kushirikiana na  Serikali.

Kwa upande wake Mtaalam Mshauri na Mdhibiti Viwango anayesimamia ujenzi wa jengo hilo Mhandisi Abdulkarim Msuya amesema kuwa jengo hilo lenye thamani
ya shilingi bilioni 11.6 linatarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.

Amesema kuwa ujenzi huo umefikia hatua za mwisho kwa asilimia 82 ambapo asilimia 18 zilizobaki ni za umaliziaji na kwamba mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anatarajia kukamilisha kazi hiyo ndani ya siku 30 hadi 45 kuanzia sasa.

Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akikagua ujenzi wa Jengo la makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mjini Dodoma.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) mfumo wa kupoza hewa alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo la NBS mjini Dodoma, ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) akipata maelezo ya ujenzi wa Makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma, alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo lenye ghorofa 5 ambalo hadi kukamilika litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akikagua ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mjini Dodoma, linalojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya na Mashirika ya Maendeleo ya nchi za Canada na Uingereza.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na miongoni mwa vijana 120 walioajiriwa katika mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, alipofanya ziara na kukagua ujenzi wa ofisi hizo, utakaogharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa, (wa tano kulia) mjini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
WAZIRI MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
https://4.bp.blogspot.com/-qnIwjEOkbCU/Wiv3i43ciwI/AAAAAAACFi4/Fp7lA0ckVTAt5Nmwzau6WzDiZtTR60DXQCLcBGAs/s640/IMG_4515.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-qnIwjEOkbCU/Wiv3i43ciwI/AAAAAAACFi4/Fp7lA0ckVTAt5Nmwzau6WzDiZtTR60DXQCLcBGAs/s72-c/IMG_4515.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/waziri-mpango-awashauri-wakandarasi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/waziri-mpango-awashauri-wakandarasi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy